Mkuu wa Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma Pololet Mgema amezindua mkakati wa kutokomeza mazalia ya mbu katika Manispaa ya Songea.
Akizungumza na wananchi katika kituo cha afya cha Mjimwema Mgema amesema Mbu waenezao magonjwa huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta umasikini katika Taifa letu kwani wengi wanaoathirika ni nguvu kazi na tegemeo katika kujenga uchumi wa Nchi Taifa.
Mgema amezitaja changamoto ambazo wanakumbana nazo ni ushiriki hafifu wa Jamii katika kushiriki kwenye usafi wa mazingira ili kuondoa uchafu ambao ni vyanzo vya mazalia ya Mbu na tabia ya jamii kutokuchukua hatua za haraka ili kupata matibabu kwenye vituo vya afya pale ambapo wamejiona wamepata maambukizi.
Kwa upande wake Afisa wa Manispaa ya Songea Vitalis Mkomela amesema kutokutumia matumizi sahihi ya chandarua na kutokuzingatia kupima vimelea kabla ya matibabu ni miongoni mwa sababu za kuendelea kwa ugonjwa wa malaria.
Mkomela ameitaja mikakati ya kutokomeza mbu hao ni kuboresha usafi wa mazingira na kujenga nyumba bora, kuwahi matibabu mapema na ,kufuata ushauri ambao unapewa na Mganga kuhusu magonjwa yaenezwayo na Mbu na kuzingatia matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu.
“Sio kila homa ni Denguee sio kila homa ni Malaria pima hakikisheni mnapima kabla y kutumia dawa”. Amesisitiza Mkomela.
Naye, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Dkt. Mameritha Basike amesema wameanzisha zoezi la unyunyuziaji dawa kwa sababu mazalia ya Mbu yameongezeka na kusababisha ugojwa wa Malaria na dengue na kwamba zoezi la kupulizia mazalia ya mbu litasaidia kutokomeza mazalia yote ya Mbu.
Vile vile amesisitiza kuwa watatoa elimu kwa Jamii kuhusu watu ambao watapita mitaani kufanya kazi ya kuuwa mazaria ya mbu.
Afisa afya wa Manispaa ya Songea Maxensius Mahungi amesema ugonjwa wa dengue umeleta madhara ya vifo katika wakazi wa mikoa 11 ugonjwa wa dengue ulianza Januari 2019 ambapo hadi Julai 15 kumekuwa na idadi ya wagonjwa 6518 na vifo sita.
Kulingana ya takwimu Wagojwa wengi wametokea Dar Es Salam 6104, Tanga 312, Pwani,57, Morogoro 22, Lindi 8, Arusha 5, Dodoma3, Ruvuma wawili katka wilaya ya Tunduru, Kagera wawili, Singida wawili na Kilimajaro mmoja.
Mahundi amesema ugojwa wa dengue unaenezwa na mbu jike aina ya aides mbu mweusi mwenye madoadoa marefu meupe ya kang’aa ambaye huuma wakati wa asubuhi,jioni na kwenye maneo yenye kivuli pia mbu denge hutaga mayai yake katika mazalio ambayo yapo kwenye kivuli cha miti ambayo ni makopo,matairi ya magari yenye maji.
Amezitaja dalili za ugojwa wa dengue kuwa ni kupata homa ya ghafra, kuumwa na kichwa hususani sehem za macho, maumivu ya viungo, kutokwa na damu sehem ya fizi, mdomoni puani na njia ya haja kubwa na ndogo, kichechefu, au kutapika, kuvumba tezi.
Imeandaliwa na
Farida Mussa
Wa kitengo cha TEHAMA Manispaa ya Songea
Septemba 18,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa