MAKUMBUSHO ya Taifa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii imejenga mnara wa kumbukumbu ya mashujaa 67 walionyongwa kikatili katika eneo la Songea klabu uliogharimu zaidi ya sh. milioni 16.
Lengo la Mnara huo ni kuwaenzi mashujaa hao ambao wakati wa uhai wao waliendeleza mapambano dhidi ya wakoloni na kuhakikisha kuwa watanzania wanajitawala wenyewe badala ya kuendelea kukandamizwa na kunyonywa na wakoloni.
Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho ya Taifa Philipo Maligisu anasema kuwa ujenzi wa mnara ni sehemu muhimu ya kumbukumbu ya mashujaa hao muhimu katika historia ya ukombozi wa nchi yetu.
Anasema mashujaa hao watakumbukwa milele kutokana na mchango wao katika ukombozi wa Tanganyika uliosababisha kumwaga damu.
Naye Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji Bartazar Nyamusya anasema ujenzi wa Mnara huo ni sehemu ya uboreshaji wa Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ya Songea ambayo sasa ina vivutio mbalimbali vya utalii wa kiutamaduni na kishujaa ambao unavutia watalii wengi wa ndani na nje ya nchi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa