Kongamano hilo limefanyika jana 19/02/2020 katika ukumbi wa Familia Takatifu uliopo Kata ya Bombambili Manispaa ya Songea;
Mgeni Rasmi katika Kongamano la wanawake Kanda ya Kusini alikuwa Mkuu Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Nyasa bi Isabela Chilumba.
Mndeme alizitaja shughuli zitakazoambatana na maadhimisho ya mwaka huu ni pamoja na makongamano katika kanda saba, misafara ya kijinsia ambapo alisema wakati wa misafara Makongamano ya kikanda yamebeba jumbe mbalimbali za kuhamasisha wanawake na jamii kwa ujumla katika kufikia Maendeleo endelevu.
“ Lengo la kongamano ni pamoja na kujadili hali ya Elimu katika Kanda ya Kusini na umuhimu wake katika Maendeleo , fursa za Uongozi kwa Wanawake pamoja na hali ya ukatili wa kijinsia katika jamii yetu ambapo washiriki watapata fursa ya kutoa michango yao na kupanga mikakati katika kufikia maendeleo ya jamii endelevu na Taifa kwa ujumla.”,alisisitiza.
Kongamano hili linafanyika katika Kanda saba ikiwemo Kanda ya Kusini ambayo inajumuisha mikoa ya Ruvuma,Lindi na Mtwara ambapo kitaifa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kitafanyika mkoani Simiyu Machi 8,2020.
UJUMBE WA KONGAMANO “ Wanawake na fursa za Uongozi ,”Ukatili wakijinsia na changamoto zake katika Maendeleo”.
IMEANDALIWA NA ;
AMINA PILLY.
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa