MRADI wa bustani ya Manispaa ya Songea umekamilika kwa asilimia zaidi ya 98 ambapo Mkandarasi tayari amekabidhi mradi huo kwa Manispaa.Mkuu wa Idara ya ujenzi wa Manispaa ya Songea amezitaja kazi zilizosalia kuwa ni kuendelea kuotesha nyasi,kufunga mfumo wa maji taka ambayo itafanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (SOUWASA) na kuweka nishati ya Umeme.
Hata hivyo amesema matazamio ya mradi huo ni miezi sita ambayo inakamilika Aprili mwaka huu na kwanba baada ya hapo Kitengo cha manunuzi kitatangaza zabuni .Mradi huo uliofadhiliwa na Benki ya Dunia umegharimu shilingi milioni 399.
ramani ya mradi huu wa aina yake katika mji wa Songea inaonesha kuwa utazungukwa na eneo la kulipia kwa ajili ya kuegesha magari,vyoo vya kulipia na vibanda vya kupumzikia.Amesema mradi huo pia utakuwa na maeneo kwa ajili ya kuchezea watoto,hoteli kwa ajli ya kupata chakula na vunywaji.Mradi huu pia unatarajiwa kuwa na eneo maalum la kupata taarifa za uwekezaji na utalii katika manispaa na mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.
“Jambo la kufurahisha ni kwamba Bustani hiyo itapandwa miti na nyasi ambazo zinaongeza mandhari nzuri na muonekano wa kuvutia wa Manispaa ya Songea kwa kuwa bustani hiyo ipo kati kati ya mji wa Songea’’,anasema
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa