Halmashauri ya Manispaa ya Songea imejengewa kitalu nyumba kimoja chenye ukubwa wa mita 30 kwa mita 8 (240m²) kwa ufadhili tokaOfisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu. Halmashauri imejenga miundombinu ya maji ili kuhakikisha maji yanapatikana kwa wakati na ya kutosha..
Wakati wa ujenzi wa greenhouse vijana 20 walifundishwa kwa nadharia na vitendo namna ya ujenzi wa greenhouse na walipatiwa vyeti.Kati ya vijana 20walioshiriki katika ujenzi, Wanaume walikua 13 na wanawake 07 ambapo miongoni mwao walemavu walikuwa 02).
Baada ya ujenzi kukamilika mkandarasi(SUGECO) aliendesha mafunzo kwa vijana ambapo vijana 99 kati ya 105 walihitimu mafunzo hayo.kati ya vijana 99 waliofundishwa kilimo ndani na nje ya greenhouse,wanaume walikua 54 na wanawake walikua 45 ambapo miongoni mwao walemavu walikua 8
Mradi huu una lengo la kuwajengea uwezo vijana 100 wenye nia ya kujiajiri kwa ajili ya kupata mafunzo ya uzalishaji wa mazao ya Mbogamboga na Matunda kwa kutumia kitalu nyumba kwa kuzingatia umri kuanzia miaka 15 mpaka 35. Idara ya kilimo kwa kushirikiana na idara ya Maendeleo ya jamii na ofisi ya Mbunge tayari imebaini vijana 100 kwa kuzingatia vigezo watakaopata mafunzo. Lakini pia watu wenye ulemavu wamepewa kipaumbele na kuingizwa katika orodha ya wanaufaika wa mradi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa