UJENZI wa kituo cha Afya Kata ya Ruvuma manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umefikia asilimia 75.Mhandisi wa ujenzi Manispaa ya Songea Karoline Bernadrd amesema hali ya ujenzi wa kituo hicho unaendelea vizuri.
Jumla ya shilingi milioni 400 ambazo zimetolewa na serikali ya awamu ya tano zinatumika katika mradi wa ujenzi wa kituo hiki.
Mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya cha Ruvuma unahusisha ujenzi wa majengo ya wodi ya upasuaji,wodi ya akinamama,wodi ya watoto, maabara, nyumba ya mtumishi na chumba cha kuhifadhia maiti.
Mwenyekiti wa ujenzi wa kituo cha Afya Ruvuma Issa Zahamba amesema ujenzi unaendelea vizuri na kwamba unatarajia kukamilika kati ya Februari na Machi mwaka huu
Kukamilika kwa mradi wa kituo hiki cha afya kutaongeza idadi ya vituo vya afya katika manispaa ya Songea hivyo kusogeza huduma za afya jirani na wananchi.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa