MRADI wa ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Ruvuma Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambacho serikali imetoa shilingi milioni 400 unatarajia kukamilika wakati wowote baada ya ujenzi wake kufikia zaidi ya asilimia 90.
Kituo hicho kikikamilika kinatarajia kutoa huduma kwa wakazi zaidi ya 45,000 wanaoishi katika kata za Ruvuma,Subira,Mateka na majengo.
Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mhandisi Karoline Bernad amesema ujenzi unaendelea vizuri ambapo hadi sasa majengo yote manne yameezekwa na kazi ya kukamilisha inaendelea.
Kulingana na Mhandisi huyo majengo ambayo yameezekwa katika mradi huo ni wodi ya mama na mtoto,jengo la upasuaji na jengo la huduma kwa watu wa nje na jengo la maabara.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa