MRADI wa maji katika Mtaa wa Ruhila kati Kata ya Mwengemshindo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma umekamilika na unatarajia kukabidhiwa kwa wananchi wa Mtaa huo Julai Mwaka huu.Mradi huo ambao umegharimu shilingi milioni 490.2 unatarajia kunufaisha wakazi 941 wa Mtaa wa Luhirakati.
Mradi wa maji Luhirakati ulianza kujengwa katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 Mkandarasi akiwa ni Berasi Investiment ambao umetekelezwa kupitia programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini .Miongoni mwa kazi zilizofanyika katika utekelezaji wa mradi huo ni ujenzi wa tanki la lita 25,000 na ujenzi wa vituo 16 vya kuchotea maji.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa