KAMATI ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetembelea mradi wa stendi kuu ya mabasi ya Songea unaotekelezwa katika Kata ya Tanga umbali wa takribani kilometa 14 kutoka mjini Songea.Kazi ambazo zinafanyika mradi huu ni ujenzi wa lami nzito kilometa mbili,taa za barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya kukatia tiketi,jengo la utawala,matundu 12 ya vyoo na eneo la kupaki magari.
Mradi huu unaotekelezwa na Mkndarasi Kampuni ya wachina ya China SICHUAN INTERNATIONAL kwa gharama ya zaidi ya shilingi biioni sita ni wa mkataba wa miezi 18 unaoanzia Machi 2018 hadi Septemba 30,2019.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa