MRADI wa ujenzi wa stendi ya kisasa ya Tanga Manispaa ya Songea ambao umeanza Mchi 25,2018 na unatarajia kukamilika Septemba 30,2018.Mradi huu katika awamu ya kwanza unagharimu zaidi ya bilioni sita ambapo tayari mradi umefikiaasilimia 30.
Kwa mujibu wa Mhandisi Mkuu wa Manispaa ya Songea Karoline Bernad,kazi ambazo zinafanyika awamu ya kwanza katika stendi hiyo ni ujenzi wa lami nzito yenye kilometa mbili,taa barabarani,maduka 30,vibanda 20 vya tiketi,jengo la utawala,vyoo vya matundu 12 na eneo la kupaki magari.Mradi huo unafadhiliwa naBenki ya Dunia ambapo hadi sasa Mkandarasi amelipwa zaidi ya shilingi bilioni 444.
Mradi hadi kukamilika unatarajia kugharimu shilingi bilioni 12 ambapo katika awamu ya kwanza, zitatumika shilingi bilioni sita na kwamba stendi mpyaya mabasi inatarajia kuanza kazi baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza yautekelezaji ambayo ni kuanzia Oktoba 2019.
Ilikuendana na kasi ya ukuaji wa mji,Manispaa iliamua kutenga eneo la kujengakituo kikuu cha mabasi kuwa Kata ya Tanga ikiwa ni umbali wa takribani kilometa14 toka mjini Songea.Kazi nyingine ambazo zitafanyika katika awamu ya kwanza napili ya mradi huo kuwa ni kujenga barabara za kuingia na kutoka stendi zenyekiwango cha lami nzito,kujenga mirefeji ambayo itapeleka majimtoni,ujenzi wa eneo la stendi lenye ukubwa wa meta za mraba 32,914,kuweka taaza barabarani katika eneo lote la stendi,eneo la utawala na kujenga majengoyenye hoteli za kisasa.
Fedhaza mradi wa stendi zimetolewa kupitia Benki ya Dunia,jumla ya hekari 15zimetwaliwa katika eneo hilo ili kupitisha stendi,ambapo shilingi milioni 38tayari zimelipwa kama fidia kwa wananchi.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa