WAZIRI wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro (MB) ameipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha huduma ya Msaada wa Kisheria Mama Samia Aid Compaion ambayo imewafikia jumla ya wananchi 1,386,656 kati ya hao wanaume 72231 na wanawake 684,425 kwa Mikoa 17.
Akizungumza Dkt. Ndumbaro (MB) alisema migogoro 14,775 imeibuliwa na kati ya migogoro 2885 imetatuliwa, migogoro 11890 inaendelea kutatuliwa ambapo migogoro ya ardhi 5474 imefuatiliwa.
Alibainisha migogoro ya ndoa 1507, matunzo ya watoto 1405, mirarhi 1277, madai mbalimbali 1225, ukatili wa kijinsia kesi 972 pamoja kesi za jinai 515 ambapo aliongeza kuwa hayo yote yamepitiwa kupitia kampeni ya Samia Legal Aid Compaign.
Amitaka jamii ikubali kubadilika tabia, maadili ili kuendelea kutenda haki bila kuvunja sheria.
Hayo yametamkwa akiwa kwenye Kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea wakati akizungumza na waandishi wa Habari tarehe 15 februari 2025.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa