Mpiga kura ambaye picha yake haipo/ haionekani katika daftari la wapiga kura lakini ana kadi ya mpiga kura yenye taarifa sawa na zilizopo katika daftari la kudumu la wapiga kura, “aruhusiwe kupiga kura kura”.
Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Songea Mjini Tina Sekambo akiwa katika ufunguzi wa mafunzo kwa makarani waongozaji wapiga kura yaliyofanyika leo 24 oktoba katika kumbi tofauti mjini Songea.
Tina amewataka Makarani waongozaji kufanya kazi kwa weredi na kwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kuacha kutumia simu wawapo kituoni ili kutoa huduma bora kwa wapiga kura sambamba na kutoa maelekezo inapobidi kufanya hivyo na kwa kutumia lugha nzuri pamoja na kuweka kipaumbele kwa makundi maalumu kama wazee, walemavu, wajawazito, wanaonyonyesha na wagonjwa.
Alisema makarani waongozaji wapiga kura ni watendaji wanaoteuliwa na msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya kuwaelekeza wapiga kura wasioweza kutambua vituo walivyopangiwa.
Aliongeza kuwa Jimbo la Songea Mjini lina vituo vya kupigia kura 393 ambapo kila karani atawajibika kuwepo kwenye kituo chake mapema kabla ya kufungua kituo ili aweze kujiandaa kutoa huduma kwa wapiga kura.
Alibainisha kuwa ili kuifahamu ipasavyo orodha ya wapiga kura, msimamizi wa uchaguzi atampatia karani mwongozo wa wapiga kura maelekezo ya namna ambavyo orodha hiyo imepangwa. Orodha hiyo itakuwa na idadi ya wapiga kura isiyozidi 450.
Aidha, moingoni mwa majukumu ya makarani waongozaji wapiga kura yaliyotajwa ni pamoja na kupokea wapiga kura nje ya kituo na kuwaelekeza eneo/ chumba watakachopigia kura, kutoa maelekezo kwa wapiga kura namna ya kujipanga katika mistari miwili kwa kuzingatia ( mstari wa wanawake na wanaume), kutoa kipaumbele kwa wenye mahitaji maalmu, pamoja na kutoa ushirikiano kwa watendaji wa kituo na mlinzi wa kituo ili kufanikisha kazi za upigaji kura kituoni. Tina Alisisitiza.
Mwisho aliwaasa makaranni hao kusimamia uchaguzi vizuri ili uwe huru na wa haki ukiwa unahusisha kuwapatia wapiga kura fursa ya kupiga kura bila kubugudhiwa wala kusumbuliwa wanapokuwa katika vituo vya kupigia kura.
MTAYARISHAJI;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
24 OKTOBA 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa