MAAMUZI ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli Kuzuia uagiza wa makaa ya mawe toka nje,badala yake watumiaji wote kutumia makaa ya mawe toka Ngaka Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma, kumesababisha soko la makaa hayo kupanda.
Meneja Uzalishaji wa Mgodi wa Ngaka David Kamenya anasema uzalishaji umeongezeka katika kasi ya ajabu toka tani 6000 hadi tani Zaidi ya 50,000 kwa mwezi hivi sasa.
Kamenya anabainisha makaa ya mawe katika mgodi huo awali yalikuwa yanapatikana mita tano chini ardhini ambapo hivi sasa baada ya uzalishaji kuongezeka madini hayo yanapatikana kati ya mita 40 hadi 50 ardhini.
Kwa mujibu wa Kamenya,makaa ya mawe yanayochimbwa katika mgodi huo yanatengenezwa kwa ukubwa wa kati ya milimita sifuri hadi 450 na kwamba hivi sasa wamepata wateja kutoka viwanda vyote katika nchi nzima kikiwemo kiwanda cha Dangote cha Mtwara ambacho kinanunua kila mwezi tani 8000 za makaa ya mawe.
“Uzalishaji wa makaa ulianza tangu mwaka 2011,eneo letu la uchimbaji lina kubwa wa kilometa kumi za mraba, utafiti wa makaa ya mawe bado unaendelea’’,anasema Kamenya.
Meneja Udhibiti Ubora wa Makaa ya Mawe wa Kampuni ya TANCOAL Bosco Mabena anasema makaa ya mawe ambayo yanazalishwa kwenye mgodi wa ngaka hayana uchafu wa aina yeyote ukilinganisha na makaa mengine nchini na nje ya nchi.
Mabena anabainisha zaidi kuwa wateja wa TANCOAL wanapendelea vipande wa makaa ya mawe vyenye ukubwa wa kati ya milimita sifuri hadi 75 na kwamba wanasafirisha makaa ya mawe toka mgodini hadi bandari kavu Kitai kwa kutumia magari aina ya tipa kabla ya kupakiwa katika magari ya mizigo na kusafirishwa mikoa mbalimbali.
“Sasa hivi tuna wateja kutoka karibu viwanda vyote vya Tanzania ikiwemo viwanda vya saruji, nguo, karatasi,jipusamu,tangu serikali ilipozuia kuagiza makaa toka nje ya nchi,sasa mambo yanakwenda vizuri kibiashara,serikali imetuwekea bajeti kubwa katika uzalishaji wa makaa yam awe ya Ngaka’’,anasema Mabena.
Utafiti uliofanywa mwaka 2008 unaonesha kuwa makaa ya mawe ya Ngaka yanaongoza kwa ubora Duniani.Katika eneo hilo zimegundulika tani milioni 400 za makaa ya mawe ambazo zinatarajiwa kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 50.
Kwa mujibu wa utafiti madini ya makaa ya mawe Ngaka yamesambaa maeneo yote ya Kijiji cha Ntunduwaro na maeneo jirani ya Kata ya Ruanda.
Ukiachia viwanda vya ndani katika nchi nzima,Tayari madini hayo yamesafirishwa katika nchi za Kenya, Zambia na Malawi.
Mgodi wa Ngaka, unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania yenye asilimia 30, na Kampuni ya Intra Energy ya Australia yenye
Katika kutekeleza Dira ya Taifa ya mwaka 2025 Tanzania inatarajia kuzalisha umeme wa makaa ya mawe ambayo yameenea katika mikoa ya kusini hususan mikoa ya Ruvuma,Mbeya Iringa na Njombe.
Sera Taifa ya madini ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi kuendeleza madini ambapo Serikali katika sera hiyo ina jukumu la kuidhibiti,kuikuza na kuiendeleza sekta hiyo.
Sekta ya madini inachangia takribani asilimia 3.5 ya Pato la Taifa,ambayo inakadiriwa kufikia asilimia 10 ifikapo 2025.
Mwandishi wa Makala haya ni Albano Midelo,mawasiliano yake ni albano.midelo@gmail.com,simu 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa