Mstahiki Meya Manispaaa ya Songea ameongoza wanachi wa kata ya Ruvuma katika zoezi la uchimbaji wa msingi wa madarasa 4 manne katika shule ya Msingi Kipera ambayo itajengwa kwa nguvu za wananchi wa kata hiyo.
Zoezi limejili kwa lengo la kuunga mkono jitihada za wananchi wa kata ya Ruvuma ambao kwa umoja wao wamekubaliana kuanzisha mchango wa ujenzi wa vyumba vya madarasa vinne 4 kwa kuchangiakiasi cha shilingi 20,000 kwa kila kaya.
Mhe. Mbano amewataka wananchi hao kuendelea kushirikiana katika kuchangia ujenzi unaoendelea kwa lengo la kupunguza changamoto ya madarasa inayoikabili shule hiyo ambapo amewaahidi wananchi hao kujenga majengo hadi kufikia hatua ya renta baada ya hapo Halmashauri itamalizia katika hatua zitakazofuata ambazo ni kuezeka na ukamilishaji.
Alisema Serikali haiwezi kufanya kazi yake bila kushirikiana na wananchi kinachotakiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuchangia nguvu kazi na michango mbalimbali kwa maendeleo ya Taifa letu.
Aliongeza kuwa Manispaa ya Songea imepokea fedha kiasi cha shilingi bil. 1.52 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarsa 76 katika shule za Sekondari kwa lengo la kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwezi januari 2023.
Kwa upande wake Mheshimiwa Diwani kata ya Ruvuma Issa Telela amewataka wananchi kuendelea kuchangia michango hiyo bila vikawazo kwa kukuwa michango iliyopangwa ni maamuzi ya wananchi wenyewe kupitia mikutano ya hadhara ya mtaa.
Alisema kukataa kuchangia kiasi kilichopangwa ni kupinga maendeleo ya kata ya Ruvuma ambapo alieleza kuwa kutokana na upungufu wa madarasa katika shule ya Msingi Kipera inawapasa kusaidia Serikali kwa kuanzisha ujenzi wa madarasa 4 manne ambayo yataishia ngazi ya Boma na baadae Serikali itamalizia.
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa