Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Mhe. Michael Mbano, amewataka waheshimiwa Madiwani kuendelea kushirikiana na wataalamu katika kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo.
Aidha Mhe,. Mbano ameagiza wataalamu kuleta taarifa za utekelezaji wa miradi kwa kila wiki ili kufuatilia kwa karibu kila hatua ya maendeleo.
Amesema “Katika tukio la ujio wa Rais DKT. Samia Suluhu Hassan, wananchi walijitokeza kwa wingi, na hili limejenga heshima kubwa kwa viongozi na jamii ya Manispaa ya Songea.
Aliongeza kuwa, Katika kutatua changamoto ya madawati Manispaa ya Songea imeweka Mkakati wa kutengeneza madawati zaidi ya 200 katika kila kata ili kukabiliana na upungufu wa madawati.
Aidha, Wataalam wa Manispaa ya Songea wameagizwa kuweka mipango ya muda mrefu na mfupi kwa ajili ya maendeleo ya mji, pamoja na kufanya mapitio ya sheria ndogo za miji ili kuhakikisha shughuli za Serikali zinaenda kama ilivyokusudiwa.
Katibu wa Tawala Wilaya ya Songea, Mtella Mwampamba, alisisitiza umuhimu wa wataalam kujitathimini kuhusu utekelezaji wa majukumu yao ambapo pia alielezea hatua zilizochukuliwa kuhusu kung’olewa kwa chuma za POSTIKODI, akiwataka wanunuzi wa chuma chakavu kuwa makini wakati wa kununua chuma chakavu pia amewataka wenye kutenda matukio hayo kuacha vitendo vya kuhujumu uchumi, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, James Mgego, aliwapongeza wataalamu kwa usimamizi mzuri wa zoezi la uandikishaji na kuhimiza Madiwani kuhamasisha wananchi kwenda kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba 2024.
IMEANDALIWA NA:
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa