MSTAHIKI Meya Manispaa ya Songea amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Sulluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Alisema Manispaa ya Songea imeendelea kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo ikiwemo na mradi wa Barabara wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bil 22, mradi wa mitaro ya maji Bil. 157, ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ya Amali unaojengwa kwa Bil. 1.6, Ujenzi wa shule ya kata ya Ruhuwiko wenye thamani ya Mil. 560, mradi wa barabara (TACTIC) zaidi ya Bil. 22 na miradi mingene yote inayoendelea kujengwa. Alipongeza.
Mhe. Mbano amewataka wajumbe wa kamati mbalimbali za kudumu zilizoundwa Mkutanoni hapo kuendelea kusimamia maadili wanapotekeleza majukumu yao ya kamati na endapo watakiuka za ya kamati hizo hana budi kuzivunja na kuunda upya ili shughuli za Serikali ziweze kusonga mbele. “Alibainisha.”
Amewataka wataalamu wa wahakikishe wanakamilisha zoezi la kuweka vibao kwenye barabara za mitaa (POST KODI) ili barabara ziweze kutambulika kwenye mitaa husika.
Ametoa kauli hizo akiwa kwenye baraza la Madiwani la mwaka 2023/2024 lililofanyika tarehe 15 August 2024 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambalo lilihudhuriwa na viongozi wa vyama vya Siasa, wataalamu na wananchi mbalimbali kwa lengo la uundaji wa kamati za kudumu za Halmashauri.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Songea Mtella Mwampamba amewapongeza viongozi waliochaguliwa wa kamati za kudumu za Halmashauri, pia alichukua nafasi hiyo kupongeza Naibu Meya ambaye amechaguliwa kwa awamu nyingi mfululizo.
Akitoa Salamu za Serikali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani ambapo aliwataka wananchi kushiriki semina ya mafunzo ya uwekezaji yanayendeshwa katika ukumbi wa Chuo kikuu Huria yanayoendeshwa na TIC ambayo yatawawezesha washiriki kupata fursa ya kujifunza namna ya kuwekeza.
Kwa upande wake katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Mjini James Mgego, amewataka Madiwani hao kuendelea kutoa ushirikiano katika kipindi cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Wakili. Bashir Muhoja alisema kwa mujibu wa kanuni 7 ambayo ni muongozo unaoeleza kazi kubwa ya mkutano wa baraza la mwaka la madiwani ni pamoja na kufanya uchaguzi wa Naibu Meya, uundaji wa kamati za kudumu za Halmashauri, uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu, upitishaji wa ratiba ya vikao vya mwaka, pamoja na uwasilishaji wa taarifa za utendaji wa kazi za mwaka uliopita.
Aidha baada ya kusoma mwogozo huo hatua za uchaguzi wa kumpigia kura mgombea Jeremia Mlembe ambaye hakuwa na mpinzani uliendelea kufanyika kwa kupigiwa kura na wajumbe ambao ni waheshimiwa madiwani 28 ambapo kura zilizopigwa ni 28, kura zilizoharibika 0, kura zilizokataliwa ni 0, na kura za ndiyo ni 28 ambapo baada ya matokeo hayo katibu wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Songea, alimtangaza Mhe. Jeremia Mlembe kuwa Naibu Meya Manispaa ya Songea baada ya matangazo ya uchaguzi huo Mkurugenzi alisoma taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ykatika kipindi cha mwaka 2023/2024.
Akitoa shukrani ya Naibu Meya Jeremia Mlembe alianza kwa kushukuru chama cha Mapinduzi ngazi ya Wilaya, Mkoa, kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Waheshimiwa Madiwani wote kwa kumchagua kwa mara nyingine mfululizo na ameahidi kutoa ushirikiano wakati wote katika kutekeleza shughuli za Serikali na Chama Tawala”. Alishukuru.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa