Imeandaliwa na;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI,
MANISPAA YA SONGEA.
Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewataka wajasiliamali wadogowadogo wote maarufu kama machinga ambao wanaendesha biashara zao katika maeneo yasiyorasmi wanatakiwa kuhama kwenye maeneo hayo na kisha kuhamia kwenye maeneo yaliyotengwa rasmi kwa ajili ya biashara za wamachinga ifikapo tarehe 31 Machi 2022.
Hayo yamebainika katika kikao na Waandishi wa habari kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea leo tarehe 29 machi 2022 kwa lengo la kueleza au kutangaza mafanikio ya utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Serikali katika kipindi cha januari hadi Machi 2022.
Mbano alianza kwa kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha Bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea ambapo fedha hizo zimesaidia katika kujenga daraja BP Stesheni, Barabara ya kiwango cha lami kutoka BP Stesheni hadi Sanga one kwa thamani ya shilingi Milioni 500, Barabara ya Seedfarm kilometa (1) moja kwa thamani ya shilingi milioni 400, pamoja na uchongaji wa barabara ya Nonga nonga hadi kata ya Tanga kwa thamani ya shilingi million 400.
Akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema “kwa awamu nyingine Manispaa ya Songea imepokea kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kurekebisha miundombinu ya barabara ikiwemo na ujenzi mpya wa daraja la Misufini - matarawe ambapo ujenzi huo utaanza mara baada ya kumalizika nyakati za masika ya mvua. Mbano “alibainisha.”
Aidha, Katika kutekeleza miradi ya Afya Manispaa ya Songea kupitia mapato yake ya ndani Manispaa ya Songea, imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Lilambo ambacho kipo hatua ukamilishaji, piatumepokea fedha Milioni 500 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Msamala ambacho kipo hatua ukamilishaji, Ujenzi wa kituo cha kituo cha Afya Subira wenye thamani ya shilingi milioni 500 fedha za TOZO ambao umefikia hatua ya ukamilishaji, pamoja na kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambao upo hatua ya utekelezaji.
Akizungumzia upande wa elimu Manispaa ya Songea ilipokea shilingi milioni 660 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 29 ikiwa madarasa 26 kwa shule za Sekondari pamoja na madarasa 3 kwa shule za Msingi ikiwa ni Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO 19,.
Ametoa rai kwa vyombo vya habari vyote kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya wazazi kuchangia chakula shuleni ili wanafunzi waweze kupata chakula shuleni ikiwa [jukumu hilo halikwepeki litabaki kuwa ni la mzazi. “Mbano alisisitiza”
Aliongeza kuwa Serikali inaendelea kutoa fedha za Elimu bila Malipo kwa ajili ya kutatua chanagamoto mbalimbali kwa shule za Msingi na Sekondari lakini haimaanishi mzazi huyo asichangie mchango wa chakula shuleni.
Mwisho, Amewataka wananchi wote wa Manispaa ya Songea kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao wanayoishi ili mazingira ya mji yawe safi.
MWISHO
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa