Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
04 MACHI 2022.
Halmashauri ya Manispaa ya Songea imefanya kikao cha Baraza la Madiwani cha kawaida kwa lengo la kupitia taarifa mbalimbali za utendaji kazi zinazofanywa ili kuleta maendeleo kwa wananchi.
Baraza hilo limefanyika hapo jana 03 Machi, 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea ambapo Baraza hilo limepitia taarifa ya utendaji kazi kutoka kamati mbalimbali ikiwemo na kamati ya fedha, utawala, uchumi, huduma za jamii, kamati ya kudhibiti UKIMWI pamoja na taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Akizungumza katika Baraza hilo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Michael Mbano amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Songea kuhakikisha anatatua changamoto zilizojitokeza katika zoezi la utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa kwenye maeneo ambayo hadi sasa fedha za miradi hiyo hazijafikishwa. ‘Alilisisitiza’
Ameitaka Menejimenti ya Manispaa ya Songea kuhakikisha inafuatilia TAMISEMI fedha za bajeti ya ujenzi wa kituo cha afya Mletele ili ziletwe kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
Mbano ametoa wito kwa waheshimiwa Madiwani kutekeleza wajibu wa kusimamia utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuleta maendeleo ndani ya Manispaa ya Songea.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa