Mstahiki meya Manispaa ya Songea Michael L. Mbano ameongoza kamati ya Fedha na uongozi katika ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 26 hadi 27 januari 2021 na kufanikiwa kukagua miradi mbalimbali ikiwemo na machinjio ya kisasa Tanga.
Awali akipokea taarifa za utekelezaji wa mradi wa Stendi mpya ya Tanga alisema “ Lengo la Serikali la kuweka mradi wa kituo cha mabasi Songea ni kuongeza mapato katika Taifa letu hususani Manispaa ya Songea ili Halmashauri iwe inauwezo wa kuwa na vyanzo vya makusanyo ya ndani kwa kutatua changamoto za wananchi kama madawati, uwekezaji kwenye zahanati, na madarasa pia alisema endapo hatuta simamia vizuri vyanzo vya mapato ya ndani hatutafanikiwa kukusanya mapato.”Mbano alisema.
Amewaasa wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria wote na madereva wote kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali na kuacha tabia ya inayoendelea kufanyika kwa baadhi ya madereva wa mabasi kukatisha safari zao na kuacha kupitia kituo cha mabasi Tanga, endapo watabainika watachukuliwa hatua za kisheria.
Amewapongeza wananchi wote wa Manispaa ya Songea kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kuchangia nguvu zao katika miradi na hatimaye Serikali kuiwezesha miradi hiyo hadi kufikia hatua ya ukamilishaji ambapo Serikali imetoa fedha za ukamilishaji/ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa nyumba ya mganga kata ya Mletele, ujenzi wa madarasa 2 chandarua Sekondari kwa Tsh 20,000,000, ukamilishaji wa vyumba vitatu vya madarasa S/m Mitendewawa Tsh 17,000,000, hosteli 1 Chabruma Sekondari na vyumba vitatu vya madarasa kwa gharama ya Tsh 138,223,235 fedha za EP4R, madarasa matatu S/m Ruhuwiko pamoja vyoo matundu tisa kwa Tsh 69,900,000 fedha za EP4R, na ujenzi wa Madarasa matatu S/m Bombambili kwa gharama ya Tsh 71,000,000 pamoja na vyoo matundu 12.
Alisema mradi wa ujenzi wa Hosteli ya chabruma Sekondari ambayo imegharimu shilingi 80,000,000 kwa ajili ya ujenzi na ukamilishaji wa mradi huo ambao umefikia hatua ya kukamilika, unapaswa kutengewa bajeti ili kuwezesha upatikanaji wa vitanda kwa ajili ya kutatua changamoto inayoikabili shule hiyo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
27 Januari 2021.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa