Na,
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
26.11.2021
Kamati ya fedha na uongozi Manispaa ya Songea, ikiongozwa na Mstahiki meya Manispaa ya Songea Michael Mbano katika ziara ya kutembelea miradi ya mpango wa maendeleo ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambayo inayoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Songea.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 26 Novemba 2021 iliyoshirikisha kamati ya fedha na wataalamu kutoka Manispaa ya Songea na kufanikisha kutembelea miradi yote inayotekelezwa na mpango wa maendelea ya Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 kwa lengo la kujiridhisha na hali halisi ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Manispaa ya Songea imepokea fedha kiasi cha shilingi milioni 660,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, miradi ambayo ipo hatua ya kuezekwa na kupigwa lipu.
Mbano amewataka wataalamu na waheshimiwa Madiwani kutoa taarifa ya maendeleo ya miradi kwa wananchi ili wafahamu hatua za miradi inayotekelezwa.
Ametoa wito kwa viongozi hao kuendelea kutembelea miradi mara kwa mara ili kuondoa changamoto mbalimbali ambazo hujitokeza.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa