Mstahiki Meya Manispaa ya Songea Michael Mbano amewwataka wananchi, Shule pamoja na Taasis mbalimbali kuhakikisha wanapanda miti kwenye maeneo yao kwa lengo la kuboresha na kuyatunza mazingira na kulinda afya za jamii.
Zoezi la uzinduzi wa upandaji miti Kiwilaya lilizinduliwa Katika kata ya Wino kijiji cha Lilondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba mnamo tarehe 01 Januari 2023 ikiwa ni utekelezaji wa kikao cha Wadau wa Misitu ambacho kilitoa maadhimio ya kufanyika kwa zoezi la upandaji wa miti ifikapo tarehe 01 Januari kila mwaka.
Akibainisha madhara yatokanayo na ukataji wa miti ovyo ni pamoja na uvutaji wa hewa ukaa, uwepo wa joto kali, jangwa, upungufu wa mvua, Saratani, njaa, pamoja na madhara mbalimbali ya kijamii na kimazingira. “ Mhe Mbano alibainisha”
Aliongeza kuwa miti ni uhai hivyo hatuna budi kupanda miti na kuitunza, pamoja na kuvuna miti kwa kufuata utaratibu uliowekwa ikiwemo na kupata kibali kutoka kwenye mamlaka husikapamoja na kudhibiti madhara ya moto yasiweze kutokea. “Alisistiza” .
Hayo yamejili wakati wa upandaji wa miti uliofanyika leo tarehe 25 Januari 2023 kaika chanzo cha Mto Ruhila ulioshirikisha wadau wa mazingira TFS, Souwasa, Waheshimiwa Madiwani, Wataalamu, pamoja na Wananchi mbalimbali kutoka kwenye kata husika.
\
Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Somgea Beno Philipo Mpwesa amesema lengo ni kuikumbusha jamii juu ya wajibu wa kuhifadhi mazingira kwa kupanda miti pamoja na kutunza vyanzo vya maji kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Beno alisema kuwa Manispaa ya Songea imejiwekea mikakati mbalimbali ya kupanda miti kila mwaka ambapo kwa mwaka 2022 ilipandwa miti 2500, na mwaka 2023 imepandwa miche ya miti 2500 katika chanzo cha mto Ruhila katika mtaa wa Unangwa kata ya Seedfarm.
Akibainisha mikakati itakayosaidia kuhifadhi na kuboresha misitu na vyanzo vya maji ni pamoja na kutoa elimu na kuhamasisha wananchi juu ya upandaji wa miti, kuendelea kushirikiana na Taasis na wadau mbalimbali katika kuhifadhi misitu, kuhamasisha na kuwaelimisha wananchoi juu ya utengenezaji wa majiko sanifu ili kupunguza kasi ya ukataji wa miti, kuanzisha bustani za miche ya miti na matunda , pamoja na kufanya doria maramara ili kudhibiti waharibifu.
Naye Godfrey Luhimbo Afisa Misitu Manispaa ya Songea alisema lengo la kupanda miti katika chanzo cha maji Ruhila ni kwa lengo la kuendeleza chanzo cha Maji SOUWASA ili mazingira yaweze kuimarika na kuepuka kutokea kwa jangwa ambalo linaweza kuathiri mazingira.
Godfrey alibainisha kuwa mwaka 2022 Manispaa ya Songea ilipanda miti 2500 ambapo kwa mwaka 2023 manispaa ya songea imepanda miti 2500 katika chanzo cha maji SOUWASA na miche ya miti 15,000 imepandwa katika shule, Mitaa 95, na kata 21.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Mtaa Kuchile Ally Shafii amesema wanaishukuru Serikali kwa kuja kupanda miti kwenye chanzo cha maji Ruhila na wameahidi kuyasimamia maeneo hayo kwa kufanya doria.
IMEANDALIWA NA
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa