Mpingo ni mti ambao umeadimika sana duniani ,miaka ya karibuni ulikuwa unapatikana kusini mwa Ethiopia na Kenya.Wataalam wa miti wanasema hivi sasa mpingo unapatikana nchini Tanzania na kaskazini mwa nchi ya Msumbiji.Inaaminika kuwa mpingo ndiyo mti wenye thamani kubwa zaidi duniani, ambapo kwa sasa unagharimu zaidi ya dola 25,000 kwa mita moja ya ujazo.
Licha ya kwamba mpingo haujawa miongoni mwa miti iliyopo hatarini kupotea duniani,unavunwa katika hali isiyokuwa endelevu.Mti huo kimataifa unawekwa kuwa moja ya Viumbehai Waliopo Hatarini Kutoweka,ambapo unaweza kupotea kabisa katika kizazi kimoja au viwili kama hakuna hatua ambazo zitachukuliwa kuuokoa.
Kwa mujibu wa Sebastian Chuwa,Mtaalam wa mimea anasema Mti wa mpingo unakua polepole na kwamba unachukua kati ya miaka 50 hadi 70 kukomaa na kuanza kuvunwa hivyo unatakiwa kuhifadhiwa.Ili kuhakikisha mti huo unakuwa endelevu,Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania imezuia usafirishaji wa mpingo nje ya nchi.Uchunguzi umebaini kuwa mti huo unaendelea kuvunwa kwa kasi kubwa kusini kwa Tanzania kwa kuwa unatumika kutengenezea vinyago.
Inakadiriwa kuwa kuna miti ya mpingo chini ya milioni tatu iliyosalia barani Afrika, mingi ikiwa nchini Tanzania na kaskazini mwa nchi ya Msumbiji.
Imeandaliwa na Albano Midelo
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa