Uchunguzi uliofanywa na Taasisi za maji za Water Laboratory Unity na Chemical and Envromental Service za jijini Dar es salaam umebaini kuwa mto huu Lunyere uliopo katika Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma una kiwango cha kutisha cha kemikali hatari ya zebaki (mercury) ambacho kimefikia kipimo cha Hg/ug 0.02.Kiwango hicho hakikubaliki kitaifa na kimataifa kwa kuwa kina madhara kwa viumbehai.
Zebaki iliyopo katika mto Lunyere inaendelea hadi Mto Ruvuma kisha kuingia bahari ya Hindi .Mto Lunyere unachafuliwa na wachimbaji wa madini eneo la Darpori mpakani mwa Tanzania na Msumbiji hali iliyosababisha mto Ruvuma pia kuathirika na zebaki.
wataalamu wanasisitiza kuwa kamwe mtu asiiguse zebaki kwa kula kupitia chakula au maji kwa kuwa zebaki ikiguswa inaingia moja kwa moja kwenye damu na ina kwenda kutua kwenye ubongo na kusababisha ubongo kusimama hivyo kuua ubongo hali inayosababisha kifo cha ghafla na magonjwa mengine kama saratani na ulemavu wa akili.
Wataalam wanatahadharisha kuwa ukila samaki wanne tu wenye zebaki unaweza kuathirika na zebaki,hata hivyo madhara hayo huchukua miaka mingi kujitokeza ndiyo maana inakuwa vigumu mtu kutambua alipata tatizo hilo lini hivyo kuendelea kutumia bidhaa ambazo zimeathirika na zebaki.
Mwandishi wa makala haya ni Albano Midelo,mawasiliano 0784765917
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa