MWANAFUNZI mmoja nchini Kenya ambaye ameongezeka katika orodha ya wavumbuzi wa magari ya nishati ya jua na uvumbuzi huo umekua kivutio katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii baada ya mwanafunzi huyo kufanikiwa kutengeneza gari linalotumia nguvu ya mwanga wa Jua(Solar Power System)
Samuel Karumbo, mwenye umri wa miaka 30, ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha Kitale Polytechnic nchini Kenya, amevumbua gari hilo katika mji wa Langas Eldoret. Gari hilo yenye siti mbili na magurudumu manne lina jopo (panel) la nishati ya jua kwa nyuma.
Baadhi ya vitu vingine vilivyopo katika mfumo wa gari gari hilo ni Kutoa asilimia sifuri ya uchafuzi wa mazingira, Jina la gari hilo ni SOLAR CAR. Gari hilo linasemekana kuwa na uwezo wa kutembea kufikia kilomita 50 kwa siku likiwa limejaa chaji.
Hii ni changamoto kwa wanafunzi wengine wa elimu Juu na wanaosoma vyuo vya ufundi fani ya Sayansi kuiga mfano wa mvumbuzi huyo na ili kwenda sanajari na karne ya Sayansi na telnolojia ambayo inabadilika kila siku.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa