Kauli hiyo imetolewa leo 08/03/2020 kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo Mh Mbunge Viti Maalm Mkoa Wa Ruvuma Jackline Msongozi.
Msongozi alisema leo ni siku pekee iliyowekwa kwa ajili ya kumkumbuka Mwanamke ambaye ni nguzo katika familia kwani pasipokuwa na mwanamke hakuna binadamu ambaye angeweza kuzaliwa hivyo mwanamke aheshimiwe duniani kote.
Awali akiwa anakagua vibanda vya maonyesho ya biashara mbali mbali uwanjani humo, aliwapongeza wanawake wajasiliamali kwa ubunifu mzuri wa kuboresha na kutunza biashara zao kwenye vifungashio ambavyo ni salama kwa walaji/wateja.
Akijibu Hotuba iliyosomwa na kaimu Afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Songea Joyce Mwanja kiongozi huyo alisema” atahakikisha anasimamia na kutetea haki, usawa na masuala ya kijinsia ambayo yanaendana sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu inayotuelekeza, na kutathimini miaka 25 tangu kupitishwa kwa azimio la Ubelgiji. Pia alikemea vikali matukio ya Ukatili kwa wanawake, unyanyasaji wa kijinsia yanayojitokeza katika jamii na kusema tabia hiyo haitakiwi katika Maisha yetu.”
Akimpongeza Mkurugenzi wa manispaa ya Songea Tina Sekambo kwa kutambua nafasi ya mwanamke katika jamii na kuweza kuwawezesha wanawake hao kwa kutoa mikopo zaidi ya mil 100 na kugawa msaada kwa watu wenye mahitaji maalum. Aidha alitoa rai kwa Taasis zinazotoa mikopo kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu ili akinamama wajasiliamali waweze kukopa na kukuza mitaji yao.
Aliwaasa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa hatari wa CORONA ambao ni tishio duniani.
Kauli mbiu ya Maadhimisho 2020” “ KIZAZI CHA USAWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA YA SASA NA BAADAYE.”
IMEANDALIWA NA ;
AMINA PILLY
KAIMU AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa