MWENGE wa Uhuru unatarajia kukimbizwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Juni 7 mwaka huu.Miongoni mwa miradi ambayo inatarajiwa kupitia na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Kibulang'oma.Kwa mujibu wa ratiba ya Mwenge wa Uhuru,madarasa hayo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40 yanatarajiwa kufunguliwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.
Miradi mingine ambayo inatarajiwa kupitiwa na Mwenge wa Uhuru ni mradi wa bwawa la samaki na utalii wa ndani Luhira katika Kata ya Msamala,Mradi wa kopa ng'ombe lipa ng'ombe uliopo kata ya Lilambo,uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga Kata ya Misufini,Uzinduzi wa zahanati ya St.Benjamini Kata ya Msamala,mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Mjimwema ambao utawekewa jiwe la msingi na mradi wa maji Mtaa wa Mitendewawa kata ya Mshangano.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa