Mkuu wa Wilaya ya Songea Kapenjama Ndile amewataka viongozi na wataalamu kushirki kikamilifu siku ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru ambao unatarajia kuwasili Manispaa ya Songea tarehe 2/04/2023 ukitokea Halmshauri ya Wilaya ya Madaba na utakabiziwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Songea katika kijiji cha Uyahudini tarehe 21/04/2023.
Agizo hilo limetolewa leo kwenye kikao kazi cha Mkuu wa Wilaya ya Songea na Watumishi wa Manispaa ya Songea kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Songea kwa lengo la kuratibu utekelezaji wa Mbio za Mwenge wa uhuru ambao utatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
Imeandaliwa na;
Amina Pilly
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa