MTAA wa Mitendewawa uliopo katika Kata ya Mshangano Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, ni mojawapo katika Mitaa 10 ya awali ambayo imetekeleza Ujenzi wa miundombinu ya maji. Mradi huu wa maji katika Mtaa wa Mitendewawa uliibuliwa na Wananchi wenyewe mwaka wa fedha 2014/2015 na kuanza kujengwa mwaka wa fedha 2016/2017 Mkandarasi akiwa ni Mkongo Building and Civil works Co.Ltd. Mradi huu unatarijiwa kukamilika Juni 30 mwaka huu,
Ujenzi wa mradi huu ulikadiriwa kugharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 517,hata hivyo hadi sasa Mkandarasi ameshalipwa zaidi ya shilingi milioni 125 ambazo zimetumika katika Ujenzi wa miundombinu ya maji.Wananchi wanatakiwa kuchangia asilimia tano ya Mradi sawa na zaidi ya milioni 25 ambayo itatumika kwa ajili ya usimamizi na uendeshaji wa mradi baada ya kukabidhiwa. Kulingana na taarifa ya mradi huo hadi sasa shilingi 124,000 zimeshakusanywa na wananchi.
Kazi zilizopangwa na kukamilika katika Ujenzi wa mradi huu ni pamoja na ;
Watu wapatao 3,200 kutoka mitaa ya Mitendewawa na wanatarajiwa kunufaika na mradi huu kwa kupata huduma ya maji safi na salama.Wananchi wanaishukuru serikali kwa kutekeleza mradi huu wa Maji ambao utasaidia wananchi kupata huduma ya maji safi na salama sehemu ya karibu na makazi yao.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 Charles Kabeho ameweka jiwe la msingi katika mradi huu ambapo ametoa wito kwa watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea na uongozi wa Chama Cha Mapinduzi Manispaa ya Songea kuhakikisha eneo ambalo limejengwa tanki la maji ambalo ni mali ya Chama Cha Mapinduzi linapata miliki kamili ili liwe chini ya serikali.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari wa Manispaa ya Songea
Juni 11,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa