Na;
AMINA PILLY;
MWANDISHI – ALAT MKOA WA RUVUMA.
23 Desemba 2021.
ALAT ni Jumuiya za Tawala za Mitaa Tanzania ambayo inatekeleza moja ya majukumu yake kama kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Serikali za Mitaa na kubadilishana mawazo, uzoefu, ujuzi baina ya wajumbe.
Katika kutekeleza hilo ALAT Mkoa wa Ruvuma ikiongozwa na Mwenyekiti wa ALAT Mkoa wa Ruvuma ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbinga Mji Mheshimiwa Kelvin Mapunda alifanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali katika Halmashauri ya Madaba iliyo jumuisha Wenyeviti wa Halmashauri zote 8 zilizopo Mkoani Ruvuma, Wakurugenzi wote, wajumbe mbalimbali wa ALAT Mkoa wa Ruvuma iliyofanyika hapo jana tarehe 22 desemba 2021.
Mh. Kelvin alisema lengo la kufanya ziara ya kutembelea miradi katika Halmashauri ya Madaba ni kukuza ufanisi na kuhimiza uwajibikaji kwenye mfumo wa Serikali za Mitaa Mkoani Ruvuma ambapo walifanikiwa kutembelea miradi ya vikundi mbalimbali vya ujasiliamali, Miradi ya Maendeleo pamoja na mradi wa uwekezaji wa kampuni Silverlands Tanzania LTD uliopo Halmashauri ya Madaba.
Aidha, baada ya kutembelea miradi ya vikundi vya wajasiliamali ALAT Mkoa wa Ruvuma walibaini baadhi ya changamoto ambazo zinakwamisha ufanisi wa utekelezaji wa vikundi hivyo ambavyo ni pamoja na upungufu wa mitaji ya kutosha kwa ajili ya kuendeshea biashara zao, Baadhi ya vikundi kukosa maeneo ya kufanyia biashara zao, pamoja na ukosefu wa elimu ya ujasiliamali kwa baadhi ya vikundi.
Katika kutatua changamoto hizo Wajumbe hao walishauri Halmashauri ya Madaba kufanya utaratibu wa kuendelea kuwawezesha wanavikundi hao ili kuinua kipato chao, pia wataalamu waisaidie jamii katika kuandaa andiko la mradi husika ambao utakuwa na bajeti halisi ya mahitaji ya kikundi chao.
Miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa madarasa matatu 3 na ofisi moja ya Walimu katika shule ya Sekondari Madaba uliojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 60 fedha za Mpango wa Maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambao ulianza tarehe 04 Novemba 2021 kwa kufuata utaratibu na muongozo wa serikalini uliotolewa na kukamilika kwa asilimia 100%.
Alisema Mamlaka za Serikali za Mitaa Mkoa wa Ruvuma zitaendelea kusimamia shughuli za maendeleo ya jamii kwa kuzingatia dira ya Taifa ya mwaka 2000 hadi 2025 kwa lengo la kuimarisha mahusiano na uwajibikaji katika Halmashauri hizo na kuimarisha uchumi wa pamoja Mkoani Ruvuma.
Amewataka Viongozi kufanyakazi kwa bidii pamoja na kushirikisha jamii katika vikao vya maamuzi na kuandaa mipango ya utekelezaji wa miradi, kusimamia ukusanyaji wa mapato kwa njia ya mifumo ili kuzuwia mianya ya uvujaji wa mapato na ubadhilifu wa fedha, kuhimiza utendaji kazi shirikishi kati ya wataalamu na madiwani ili katika tafsiri ya uhalisia wa utekelezaji wa miradi ambao ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Naye katibu wa ALAT Mkoa wa Ruvuma Grace Quintine ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Mji aliwapongeza wataalamu wote wa Halmashauri ya Madaba kwa kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa madarasa ya Mapango wa Taifa na mMapambano dhidi ya UVIKO 19 ambao umetekelezwa kwa 100% na kwa wakati uliopngwa na Serikali.
Quintine ametoa rai kwa walimu wa shule mbalimbali ambao wameshiriki kusimamia ujenzi wa madarasa hayo kusimamia miundombinu ya shule ili isiweze kuharibiwa na wanafunzi.
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa