ALAT ni Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania ambayo iliundwa kikatiba mwaka 1984 Desemba na kuanza kutumika rasmi mwaka 1985 kwa lengo la kupigania haki za Halmashauri na kuwa sauti moja katika kuleta maendeleo ya Halmashauri na kufanya mawasiliano ya karibu na Serikali kuu.
Aidha, ni Chombo kinachowezesha kukuza maendeleo ya Serikali za Mitaa zilizo huru na kutoa mchango katika kupeleka madaraka kwa wananchi, kuwasaidia madiwani, Mameya na wenyeviti katika majukumu yao kama wawakilishi waliochaguliwa kidemokrasia ambacho kinatoa uongozi, kuhimiza, kukuza ufanisi, uhuru, uwajibikaji, uwazi na demokrasia kwenye mfumo wa Serikali za Mitaa Tanzania na kwingineko duniani.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Ruvuma Mheshimiwa Kelvin Mapunda alisema “ anamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha nyingi za miradi kwenye Halmashauri Mkoani humo, ambapo amewataka viongozi hao, kuhakikisha wanasimamia utekelezaji wa miradi hiyo inayoendelea kujengwa kwenye Halmashauri mbalimbali na pia wahakikishe miradi hiyo inakamilika kwa wakati.”
Ametoa Rai kwa viongozi wa Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kusimama imara katika kukusanya mapato ya Halmashauri kwa lengo la kuleta maendeleo yenye tija kwenye Halmashauri zao. “ Mhe. Kelvin alisisitiza”
Aliongeza kuwa, Umoja na Mshikamano katika utendaji kazi ni nguzo ya Msingi hivyo amewataka wajumbe hao kuendelea kudumisha ushirikiano hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Akitoa pongezi kwa Wakurugenzi wote Mkoani Ruvuma, kuendelea kushirikiana katika Jumuiya hiyo ambayo inawawezesha kufanyika kwa vikao vyote vya kikatiba ndani ya mwaka husika ambapo amesema kufanyika kwa vikao hivyo kunapelekea Halmashauri kupata mafanikio ya kiutendaji ambapo pia amezitaka Halmashauri zote Mkoani Ruvuma kwenda kujifunza Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika namna ya uendeshaji wa Biashara ya Kaboni. “Alisisitiza.”
Kikao hicho kimefanyika katika Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma tarehe 19/08/2024 katika ukumbi wa Wilaya ya Tunduru ambacho kilihudhuriwa na Wajumbe wa Jumuiya hiyo kutoka kila Halmashauri Mkoani Ruvuma kwa lengo la kufanya ufutiliaji wa utekelezaji wa shughuli na kujadili taarifa mbalimbali za maendeleo ambacho hufanyika kila robo moja ya mwaka.
Wakizungumza na chanzo hiki cha habari, wajumbe hao wamesema”wanamshukuru Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma kwa kutoa kibali cha kufanyika kwa vikao vya kamati hiyo, ambavyo vinawasaidia kukutana kwa pamoja na kujadili maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kupitia Halmashauri zao, ikiwemo na mafanikio ya Ziara ya Katavi ambayo wajumbe hao, walijifunza namna ya uendeshaji wa Biashara ya Kaboni ambapo wameahidi kuyafanyia kazi kwa vitendo.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
ALAT RUVUMA.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa