Miche ya Miti 350 imepandwa katika viwanda vidogo Lilambo, Kituo cha Afya Lilambo, na Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM miaka 46 ambayo huadhimishwa ifikapo tarehe 05 Februali ya kila mwaka.
Uzinduzi wa maadhimisho hayo umefanyika tarehe 28 Januari katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika kata ya Tanga ambayo imeadhimishwa kwa kutembelea miradi ya Maendeleo na kujionea uhalisia wa hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi.
Ziara hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Komredi Oddo Mwisho ambayo itahitimishwa siku ya kilele katika Wilaya ya Tunduru tarehe 05 Februari ikiwa na lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na uwekezaji wa viwanda vidogo Kata ya Lilambo ambapo vikundi 11 vilikopeshwa zaidi ya Mil. 465 iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba na ununuzi wa vitendea kazi, ujenzi wa kituo cha afya kata ya Lilambo uliojengwa kwa gharama ya Mil 500 fedha za mapato ya ndani ambao umeanza kutoa huduma ya awali.
Miradi mingine iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa barabara ya HEROES hadi Mjimwema km 1 kwa gharama ya shilingi Mil. 500 fedha kutoka Serikali kuu ambao ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020 ya CCM ibara ya 57 ikiwa na lengo kuu la kuboresha miundombinu ya usafirishaji na uchukuzi katika kuwezesha shughuli za kiuchumi na kijamii mijini na vijijini.
Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwa gharama ya shilingi Mil. 500 ambapo mradi upo hatua ya ukamilishaj, ujenzi wa madarasa 6 shule ya Sekondari Lizaboni, ujenzi wa vyumba vya madarasa 4 shule ya Sekondari Lukala pamoja na upandaji wa miti 100 katika Kiwanda kidogo Lilambo, miche ya miti 100 katika Kiituo cha Afya Lilambo na upandaji wa miche 150 katika Hospitali ya Manispaa ya Songea.
Mhe. Mwisho amewataka viongozi ngazi ya Kata na matawi kushirikiana na Maafisa watendaji wa kata na Mitaa katika kutatua suala la wanafunzi wasioripoti shule wa kidato cha kwanza ili kufanikisha Lengo la Serikali la kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza lazima aripoti shule.
Ametoa Rai kwa Manispaa ya Songea kuhakikisha viwanda vidogo vilivyopo katikati ya Mji vihamishiwe kata ya lilambo katika eneo dogo la viwanda, pamoja na kuboresha miundombinu inayozunguka eneo la viwanda hususani Barabara.
Amewapongeza wataalamu wa Manispaa ya Songea kwa kujenga kituo cha afya Lilambo kilichojengwa kwa fedha za mapato ya ndani ambapo kwasasa kimeanza kutoa huduma za awali pamoja na hatua nzuri za utekelezaji wa miradi ya maendeleo. “MHE. Oddo alipongeza.”
“Amewataka Wataalam wote kuhakikisha wanasimamia na kutunza miti iliyopandwa siku ya uzinduzi wa maadhimisho hayo ili kutimiza lengo la Ruvuma kuwa ya kijani.” Amesisitiza.
Aidha, katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa chama cha Mapinduzi miaka 46, kwa Songea mjini wameweza kusajili wanachama wapya 906.
IMENDALIWA NA;
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa