Mwenyekiti wa kamati ya Ushauri ya wanawake TALGWU Mkoa wa Ruvuma bi Anna Mputa akiongoza kikao cha wajumbe wa kamati hiyo na kusikiliza kero mbalimbali zinazohusu wanawake wanachama wa TALGWU na changamoto mbalimbali za watumishi wa chama hicho kilichofanyika katika ofisi ya TALGWU Mkoa wa Ruvuma tarehe 09.04.2021.
Alisema wanachama wanawake wanachangamoto nyingi hivyo amewataka wajumbe hao kufanya ziara ya kuwatembelea watumishi kwenye maeneo yao sambamba na kutoa elimu ya wajibu wa mtumishi mahala pa kazi ili kuondoa migongano na waajili.
Alisema Chama cha TALGWU kinaelekea kwenye uchaguzi hivyo kila mmoja wao anatakiwa kuhamasisha wanachama kujitokeza kushiriki kwenye uchaguzi mara muda utakapowadia.
Alisema taratibu za ugawaji fomu kwa wagombea zilitolewa na uongozi ngazi ya Mkoa hivyo amewaasa wanachama wanawake kujiamini wakati wakugombea nafasi mbalimbali pamoja na kutokata tamaa mapema kwani kila mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yoyote chamani. Chama hicho kinatarajia kuanza uchaguzi hivi karibuni mara baada ya taratibu za kiutendaji kukamilika.
Naye Mwenyekiti wa TALGWU Mkoa wa Ruvuma Willy Luambano alisema mwaka huu Sherehe za Mei Mos zitafanyika kimkoa katika Wilaya ya Nyasa, hivyo amewataka wanachama wa TALGWU kushiriki kwenye maadhimisho hayo ili kujenga umoja na mshikamano chamani.
Mwisho alimaliza kwa kusema TALGWU - CHAMA IMARA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
13.04.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa