NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ramadhan Kailima amewataka wataalamu Mkoani Ruvuma kuhakikisha wanafuta HOJA za ukaguzi kwa kila Halmashauri ifikapo disemba 2022.
Hayo yamejili katika kikao kazi cha utekelezaji wa maagizo ya LAAC “ Local Authority Accounting Comettee” kilichofanyika leo tarehe 14 Novemba 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na Wakurugenzi kutoka kila Halmashauri Mkoani Ruvuma pamoja na wakuu wa Idara mbalimbali kwa lengo mahususi la kupata taarifa za utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na kamati ya LAAC.
Ndugu Kailima alisema kuwa, lengo la kutembelea Mkoa wa Ruvuma ni kwa ajili ya kushiriki kikao kazi na kupokea taarifa ya utekelezaji wa HOJA za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali pamoja na maagizo ya kamati ya LAAC ambapo amewataka wataalamu wote kila Halmashauri kuhakikisha wanajibu Hoja zote za Ukaguzi .
Alisema Hoja zilizosalia kipindi cha miaka ya nyuma Mkoani Ruvuma zilikuwa 114 kati ya hizo Hoja 84 zimefungwa ambapo HOJA 30 bado hazjajibiwa pia katika mwaka wa fedha 2020/2021 Mkoani Ruvuma kumekuwa na Hoja mpya 228 kati ya hizo Hoja 138 zimefungwa, Hoja 90 bado hazijajibiwa, na kufanya kuwa na jumla ya hoja ambazo bado hazijajibiwa 120 ambapo ameagiza kufutwa kwa hoja hizo ifikapo disemba 2022. “Kailima amesisitiza.”
Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma Stephen Mashauri Ndaki alisema katika kufanikisha kusimamia maagizo yaliyotolewa ya HOJA za Ukaguzi, ambapo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa imetoa maelekezo kwenye Halmashauri zote 8 na kuhakikisha taarifa hizo zinawasilishwa pamoja na uzingatiaji wa sheria mbalimbali za kutangaza kupitia gazeti la Serikili.
Kwa upande wa Halmashari ya Manispaa ya Songea katika ukaguzi wa hesabu kwa mwaka 2020/2021 na miaka ya nyuma kulikuwa na Hoja za ukaguzi 61 kati ya hizo Hoja zilizofungwa 47,na kusalia hoja 14 pamoja na maagizo 3 ambayo yametekelezwa sawa na asilimkia 100% ambapo kwa mwaka 2020/2021 Halmashauri hiyo ilifanikiwa kupata HATI INAYORIDHISHA.
AMINA PILLY;
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa