NAIBU Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu kufanya mazungumza na Wakala wa Ujenzi Tanzania (TBA) kutokana na kusuasua kwenye miradi ya ujenzi ya Wizara hiyo ikionekana inafaa kuvunja mkataba na TBA.
Ametoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa toka kwa mkuu wa shule ya Sekondari ya wasichana Songea Tupoke Ngwala ilionesha kuwa ukarabati wa mabweni unasuasua hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo ambao ni zaidi ya 800.Naibu Waziri wa Elimu alikuwa katika ya ziara ya kikazi ya siku mbili wilayani Songea na Namtumbo mkoani Ruvuma.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa