Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Massanja amewataka Wananchi kuwaenzi viongozi wa mashujaa pamoja na kuhifadhi mila na tamaduni zetu ambazo yatupasa kulinda, kuondoa uadui, ujinga, kupambana na ujangili wa wanyama pori, kupinga madawa ya kulevya pamoja na kupinga unyanyasaji wa kijinsia.
Amewataka kutumia na kutunza kumbukumbu za kihistoria ambazo zinaweza kutumika kuanzisha matamasha mbalimbali ambayo yatasaidia kuhifadhi urithi wetu kutoka kizazi kimoja kwenda kizazi kingine pamoja upatikanaji wa fursa ya ajira ambazo zitaongeza kipato kwa jamii ikiwa maadhimisho hayo yataratibiwa vizuri.
Hayo yamejiri katika kilele cha maadhimisho ya 118 ya mashujaa wa vita vya majimaji ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 27 Februari ya kila mwaka ambyo yalihudhuriwa na wadau mbalimbali wa maakumbusho wa mashujaa, Viongozi, na wanachi kwa lengo la kuwaenzi mashujaa waliojitoa mhanga katika kupigania, Haki, Uhuru na amani katika Taifa letu iliyofanyika katika uwanja wa mashujaa Songea.
Mhe. Mary alisema Serikali imekuwa ikipokea taarifa kuwa kuna mali kale ambazo zilichukuliwa ikiwemo na fuvu la Songea Mbano ambapo katika kutekeleza taarifa hiyo Serikali imeunda kamati ya kitaalamu ya kuratibu kazi na kubaini mali kale zilizopo nje ya Nchi ili kuandaa mpango wa kurejesha na kuzifanya ziwe kumbukizi. “Alibainisha”.
Aliongeza kuwa Historia ya Tanzania haiwezi kukamilika bila kuwataja mashujaa wa vita vya majimaji ambao walijitoa uhai wao kwa kupinga uvamizi wa Tawala za kikoloni ambapo Mashujaa hao walitumia mbinu za asili dhidi ya wakoloni waliokuwa na silaha Imara ambapo pamoja na kushindwa vita hivyo walipanda mbegu ya Utaifa, Uzalendo, Ukakamavu, Amani, na Upendo katika Taifa Letu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Kapenjama Ndile ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Songea alisema “Maadhimisho hayo yanatoa fursa kwa wadau kushiriki, kujadili, kutembelea na kuonesha vivutio vya Utalii vilivyoko Tanzania hususani Mkoa wa Ruvuma.”
Ndile alibainisha kuwa maadhimisho hayo yalizinduliwa tarehe 25 Februari ambapo zilifanyika shughuli mbalimbali ikiwemo na mkesha wa shughuli za kitamaduni, burudani, maonesho ya vyakula vya asili, kufungua Ukumbi wa Historia, Uzinduzi wa uboreshaji wa Makumbusho ya Majimaji baada na Kabla pamoja na kitabu cha Kihistoria na mdahalo uliofanyika katika Wilaya ya Tunduru.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Vita vya Majimaji Dkt. Noel Luoga alisema baada ya kupata Uhuru Baba wa Taifa kupitia kamati ya chama cha TANU 1965 alipitisha azimio la kujenga Minara ya kudumu ya kumbu kumbu ya mashujaa wote katika maeneo ya Kihistoria ya chimbuko la kupigania Uhuru.
Dkt. Luoga alibainisha kuwa, katika kutekeleza azimio hilo Mamlaka ya Mkoa wa Ruvuma iliamua kujenga Makumbusho ya Majimaji katika eneo ambalo walizikwa Mashujaa 67 wa vita vya Majimaji na baada ya kukamilika ujenzi yalifunguliwa rasmi na Baba wa Taifa Mwl Julius K. Nyerere tarehe 06 Julai 1980.
KAULI MBIU;
“MAKUMBUSHO YA MAJIMAJI NI URITHI WETU KWA MAENDELEO YA UCHUMI NA UTALII.”
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa