Miongoni mwa wataalamu waliosimamia vizuri miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule ni pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Songea “ hongereni sana.”
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mh. David Ernest Silinde (MB) akiwa ziarani Manispaa ya Songea leo tarehe 24 februari 2021 ambapo ameweza kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ya miundombinu ya shule za Sekondari na kujionea ufanisi mkubwa wa utekelezaji wa miradi hiyo.
Mh. Silinde (MB) alisema lengo la ziara hiyo ni kukagua matumizi sahihi ya fedha za Serikali (EP4R) na kujiridhisha kama fedha iliyotolewa imeendana na thamani halisi ya mradi uliokusudiwa ambapo Serikali ilitoa fedha Tsh milioni 80,000,000 shule ya Sekondari ya Mdandamo pamoja na Sekondari ya Chabruma kwa ajili ya kujenga mabweni.
Aliongeza kuwa mwaka 2021 Serikali imeweka mpango wa kujenga Sekondari 1000 mpya, pamoja na ujenzi wa Sekondari 26 yaani kwa kila Mkoa utakuwa na sekondari moja za wasichana ili kuwaondolea changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Alisema kuna baadhi ya Halmashauri nyingine zimepewa fedha nyingi za mradi lakini wameshindwa kutekeleza mradi ipasavyo kutokana na kujiongezea gharama za manunuzi na kudai kuwa fedha hizo hazitoshi “kwa fedha za Serikali huo ni wizi”
Akitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea, Mhandisi wa Ujenzi wa Manispaa, wakuu wa shule zenye miradi hiyo, kwa usimamizi mzuri wa miradi ya ujenzi wa Bweni katika shule ya Sekondari Mdandamo pamoja na Sekondari ya Chabruma na kusisitiza kuwa wataalamu hao ni mfano wakuigwa.
Mh. Silinde amehitimisha ziara yake leo katika halmashauri ya Manispaa ya Songea na kuendelea na ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya Songea na Mbinga.
IMEANDALIWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
24.02.2021
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa