NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Josephat Sinkamba Kandege anatarajia kuanza ziara katika mkoa wa Ruvuma kuanzia Agosti 10 hadi 14 mwaka huu.Akiwa katika mkoa wa Ruvuma,Kandege anatarajia kutembelea na kukagua kituo cha Afya Madaba na Mtyangimbole katika Halmashauri ya Madaba wilayani Songea.
Kulingana na ratiba ya zaira hiyo Naibu Waziri huyo wa TAMISEMI akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea anatarajia kukagua miradi ya ujenzi wa stendi ya kisasa na machinjia katika Kata ya Tanga,mradi wa kituo cha Afya kata ya Ruvuma na mradi wa barabara za lami mjini Songea na kwamba atafanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Songea na kukagua vituo vya Afya Muhukuru,Mchoteka na zahanati ya Lugagara
Waziri Kandege katika wilaya ya Mbinga anatarajia kukagua kituo cha Afya Kalembo,katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa anatarajia kukagua mradi wa kituo cha Afya Mkili,katika wilaya ya Namtumbo anakagua kituo cha Afya Namtumbo,katika wilaya ya Tunduru atatembelea na kukagua vituo vya afya Matemanga na Mkasale.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri pia atapata fursa ya kuzungumza na watumishi katika kila Halmashauri.
Kulingana na ratiba hiyo Agosti 10,2018 atakuwa katika Halmashauri za Madaba na Songea Manispaa wilaya ya Songea .Agosti 11 atakuwa katika wilaya ya Mbinga na Nyasa,Agosti 12 na 13 atakuwa katika Halmashauri ya wilaya ya Songea na Agosti 14 anatarajia kumaliza ziara yake katika wilaya za Namtumbo na Tunduru.
imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
Agosti 8,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa