Taasis ya kuzuia na kupambana na rushwa ( TAKUKURU) ni chombo kilichopewa dhamana kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11, ya mwaka 2007 ya kuongoza vita dhidi ya rushwa na ufisadi nchini.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma Hamza Mwenda katika kikao na Waandishi wa Habari ambacho hufanyika kila baada ya robo ya mwaka ambapo husomwa taarifa ya utendaji kazi na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miezi mitatu kilichofanyika katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma 23 oktoba 2020.
Mwenda alisema katika kipindi hicho TAKUKURU Mkoani Ruvuma ilipokea jumla ya taarifa 160 kutoka kwa wananchi kupitia vyanzo mbalimbali ambapo idara zilizolalamikiwa ni vyama vya siasa 35 (rushwa kwenye kura za maoni), Serikali za mitaa 24( watendaji wa kutosoma taarifa za mapato na matumizi na kufanya ubadhilifu wa fedha za vijiji), taasis za fedha 20, Ardhi 20, na polisi 11, Elimu 7, mahakama 5, biashara 4, afya 4, misitu 4, mifungo 3, maji 2, madini 2, sheria 2, kilimo 3, ushirika 1, viwanda 1, usafirishaji 1, na nishati 1.
Aliongeza kuwa TAKUKURU Mkoani Ruvuma imefanya kazi ya uchambuzi wa mfumo wa ukusanyaji wa ushuru wa huduma (service leavy) Wilayani Namtumbo na Nyasa na kubaini Halmashauri kutokusanya Zaidi ya kiasi cha shilingi milioni 36 kutoka kwa kampuni 18 zilizofanya kazi chini ya TARURA na TANROADS.
Aidha, TAKUKURU Mkoani Ruvuma imefanya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo nane “8” yenye thamani ya bilioni 3 tatu kwa lengo la kujiridhisha iwapo fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo zinaendana na thamani halisi ya utekelezaji wa miradi katika sekta ya maji, barabara, na elimu ambayo ni mradi wa barabara ya lami kilosa-bomani-ikulu mpya wilayani Nyasa wenye thamani ya milioni 474,427,000, mradi wa RUWASA wenye thamani ya milioni 390,870,000.
Mradi wa upanuzi na ukarabati wa mradi wa maji kijiji cha namasakata Wilayani Tunduru wenye thamani ya shilingi 147,154,975, mradi wa ujenzi wa madarasa matatu “3” shule ya msingi Mlingoti wenye thamani ya milioni 60,000,000, mradi wa ujenzi wa matundu 19 ya vyoo vya wanafunzi shule ya msingi mwenge Wilayani Namtumbo wenye thamani shilingi milioni 28,517,086, mradi wa maji mtiririko Mkongo Gulioni-Nahimba wenye thamani ya shilingi milioni 2,069,575,521.
Akiitaja miradi mingine iliyofuatiliwa na TAKUKURU Mkoani Ruvuma ni ujenzi wa tanki la maji la Lusaka Mbinga Mjini lenye ujazo wa 500m3 lililogharimu shilingi 200,135,522, pamoja na mradi wa wa maji kijiji cha Myangayanga Mbinga Mji wenye thamani ya shilingi 35,220,396. “Mwenda alisema.”
Hata hivyo aliwaeleza waandishi wa Habari kuwa TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma imeendelea kutekeleza jukumu la kushirikisha na kuelimisha jamii katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kufanya semina 69, mikutano ya hadhara 30, klabu 54 za wapinga rushwa mashuleni , Makala 2, redio 14 pamoja na Website za Halmashauri.
Mwisho, aliitaja mikakati waliyojiwekea kuelekea katika kipindi cha Kampeni za wagombea wa vyama vya siasa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi ili wafahamu umuhimu wa uchaguzi, lengo la uchaguzi, sheria zinazoongoza uchaguzi, umuhimu wa kupiga kura, na thamani ya kura.
Alimaliza kwa kutamka “Mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu letu wote”
IMETAYARISHWA NA;
AMINA PILLY;
AFISA HABARI MANISPAA YA SONGEA.
23 OKTOBA 2020.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa