BENKI ya NMB imetoa msaada wa kitanda kimoja cha kuzalia,vitanda vine vya kulala wagonjwa,na shuka ( 49) Msaada wenye thamani ya shilingi milioni tano katika Kituo cha afya cha Mbamba-bay katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Akizungumza kabla ya kukabidhi msaada huo katika Kituo hicho cha Afya Mbamba-bay, Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Janeth Shango amesema kwa miaka kadhaa sasa NMB imekuwa mstari wa mbele kuchangia miradi ya mbalimbali ya maendeleo.
“Mpaka ninavyoongea leo, kwa mwaka huu 2019 pekee,tayari tumetoa misaada yenye thamani ya shilingi milioni 710,tumejikita zaidi kwenye miradi ya elimu na afya na majanga mbalimbali yanayotokea katika jamii’’,amesema Shango.
Hata hivyo amesema katika miradi ya elimu NMB imejikita katika madawati na vifaa vya kuezekea na katika sekta ya afya wamejikita kwenye vitanda na magodoro yake .
Kulingana na Meneja huyo wa NMB Kanda ya Kusini,kwa mwaka 2019 Benki hiyo imetenga bajeti ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii katika sekta ya elimu na afya na majanga mbalimbali.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika Hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba ametoa rai kwa watanzania kuitumia Benki ya NMB kwa kuwa imezifikia wilaya zote nchini kwa asilimia 100 na kwamba inatoa huduma za kibenki kwa mitandao ambazo zinapatikana kwa wananchi wengi zaidi mijini na vijijini.
“Mimi kama Mkuu wa Wilaya kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Nyasa nawashukuru NMB kwa msaada wenu ambao mmekuwa mnautoa kwetu mara kwa mara kwa maana tulihangaika sana kutafuta wadau mbalimbali kwa ajili ya kukiendeleza kituo chetu cha afya cha Mbamba-bay kwa kuwa muda mrefu kimekuwa kikitoa huduma kama Hospitali ya Wilaya ya Nyasa kwa kuwa hatukuwa na Hospitali ya Wilaya mpaka pale Mh Rais Dkt John pombe Magufuli opalipotujengea Hospitali ya Wilaya ya Nyasa ambayo haijaanza kutumika.’’,alisema Bi Chilumba.
Hata hivyo amesema NMB imekuwa msaada mkubwa katika wilaya ya Nyasa ambapo mwaka 2018 walitoa msaada wa mabati katika shule ya msingi kilosa na Shule ya Sekondari Monica Mbega iliyopo katika Kata ya Mbaha Wilayani Nyasa.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Douglas Ruambo, alisema msaada huo umekuja wakati mafaka kwa kuwa Kituo hicho cha afya kilikuwa na upungufu wa vifaa hivyo ambavyo Nmb wametatua changamoto hizo..
Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa wa kituo cha afya Mbamba-bay ameishukuru Benki ya NMB kwa msaada huo ambao amesema unakwenda kutatua changamoto ya vifaa hivyo na kuongeza utoaji huduma bora kwa wananchi kwa kuwa kwa sasa Kituo hicho cha Afya Mbamba-bay kinapokea Wagonjwa kutoka Wilaya ya Mbinga na Songea kutokana na Ubora wa huduma za afya zinazopatikana katika Wilaya ya Nyasa.
Imeandaliwa na Netho c. sichali kaimu afisa habari Wilaya ya Nyasa 0767417597
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa