UNAPOSEMA chakula hiki siwezi kula,wenzako chakula cha aina hiyo wanaona ni sawa na kupata dhahabu kwa sababu kinagombaniwa kutokana na madai kuwa ni kitamu Zaidi ya vyakula unavyovijua.
Baadhi ya wananchi wa wilaya ya Masasi mkoani Ruvuma wagombani kitoweo cha nyama ya panya wakidai kuwa nyama hiyo utamu wake unazidi nyama ya kuku n ahata samaki maarufu .
Utegaji na uuzaji wa panya umekuwa ukiwanufaisha baadhi ya watu katika Kijiji cha Chikoweti wilayani Masasi mkoani Mtwara.
Kijiji hicho kinakaliwa zaidi na watu wa kabila la Kimakua ambao wamekuwa na historia ya kutumia panya katika maisha yao ya kila siku kama kitoweo muhimu katika mlo.
Kwa upande wake Martha Mkuti anasema ulaji wa panya ni wa mazoea kutokana na kutokuwa na kitoweo mbadala katika maeneo wanayoishi.
“Ni kweli ladha ya panya ni kama samaki ndio maana tunaridhika kula, wapo watu wanaunga kwa nazi, ni watamu mno na wengine hupenda kula chukuchuku,huwezi kumfananisha na kiumbe mwingine wala kuku, yaani panya ukishamkamata unamchoma na ana mafuta ya kujitegemea ila unaongeza chumvi tu,” anasema Minjale.
Mzee Mpupua ambaye anajishughulisha kutengeneza mitego ya panya, anasema kazi hiyo ameifanya kwa zaidi ya miaka 36.
Uchunguzi umebaini Kitoweo cha panya huuzwa kwa mafungu ya panya watano kwa Shiingi 500 na fungu lingine ambalo huwa na panya wanane ambao ni wakubwa huuzwa hadi shilingi 1,000
Ofisa Lishe Mkoa wa Mtwara, Herieth Kipuyo, anasema ulaji wa nyama una faida kubwa kwenye mwili wa binadamu kwa kuwa mnyama huyo yupo katika kundi la vyakula vyenye protini.
Makala imeandikwa na Albano Midelo kwa msaada wa mitandao ya kihabari
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa