Nyotamkia(kimondo) ilichomoka angani kutoka katika orbiti yake na kuanguka mwaka 1840 katika Kijiji cha Ndolezi Wilaya ya Mbozi Mkoa mpya wa Songwe kusini mwa Tanzania,ni kivutio adimu duniani.Nyota hiyo yenye uzito wa tani 12 ni ya nane kwa ukubwa kati ya nyotamkia 600 zilizoanguka Duniani.
Mwaka 1930 watalaam wa kijerumani walikata kipande ambacho walikipeleka Ujerumani na kubaini nyotamkia hiyo ina aina tano za madini ambazo ni chuma,nickel,shaba,sulphur na fosforas.Nyota hiyo ndiyo ya kwanza kwa ubora Duniani.Katika eneo la Peramiho mkoa wa Ruvuma inaaminika pia kuna nyotamkia ndogo ilianguka mwaka 1899.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa