Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 13 Agosti, 2018 amefanya uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 41, na amewahamisha vituo vya kazi Mkuu wa Wilaya 1 na Wakurugenzi wa Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji 19. Taarifa iliyotolewa leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Dkt. Magufuli amemteua Bi. Senyi Simon Ngaga kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kwimba Mkoa wa Mwanza.Bi. Senyi Simon Ngaga amechukua nafasi ya Mhandisi Mtemi Msafiri Simeon ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Mkoani Geita, baada ya Mkuu wa Wilaya ya Chato aliyeteuliwa hivi karibuni Kanali Patrick Norbert Songea kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi nje ya nchi.Uteuzi wa Bi. Senyi Simon Ngaga unaanza leo tarehe 13 Agosti, 2018 na Wakuu wa Wilaya wote wawili wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi mara moja.AIDHA, Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi na uhamisho wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji, kufuatia baadhi ya Wakurugenzi waliokuwa katika nafasi hizo kustaafu, kupangiwa kazi nyingine, kuhamishwa na wengine kuondolewa katika nafasi za ukurugenzi kama ifuatavyo;1. Mkoa wa Arusha.i. Jiji la Arusha – Dr. Maulid Suleiman Madeni.ii. Halmashauri ya Wilaya ya Meru – Bw. Emanuel Mkongo.2. Mkoa wa Dar es Salaam.i. Manispaa ya Temeke – Bw. Lusubilo Mwakabibi (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma).ii. Manispaa ya Ubungo – Bi. Beatrice Dominic Kwai (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara).iii. Manispaa ya Ilala – Bw. Jumanne Kiango Shauri (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Korogwe).iv. Manispaa ya Kigamboni – Bw. Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa).3. Mkoa wa Dodoma.i. Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa – Bw. Mustafa S. Yusuph.ii. Halmashauri ya Mji wa Kondoa – Ndg. Msoleni Juma Dakawa.iii. Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa – Bw. Paul Mamba Sweya.iv. Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa – Dkt. Omary A. Nkullo.4. Mkoa wa Geita.i. Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale – Bi. Mariam Khatib Chaurembo.ii. Halmashauri ya Wilaya ya Chato – Bw. Eliud Leonard Mwaiteleke (Amehamishiwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
Imetolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa