PATO la Mkoa wa Ruvuma(Regional Domestic Product-GDP) limeongezeka toka shilingi 3,544,392,000,000.00 mwaka 2015 hadi kufikia shilingi 4,046,849,000,000.00 mwaka 2016.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amesema ongezeko hilo ni sawa asilimia 87.6 na kwamba pato la Taifa kwa mtu(Per capital income) kwa mwaka 2015 katika Mkoa wa Ruvuma lilikuwa shilingi 2,415,486 na kwamba limeongezeka hadi kufikia shilingi 2,700,022 mwaka 2016 sawa na ongezeko la asilimia 11.8.
Hata hivyo Mndeme amesisitiza kuwa uchumi wa Mkoa wa Ruvuma hutegemea kilimo ambapo zaidi ya asilimia 87 ya wakazi wake hupata riziki yao kupitia kilimo na kuchangia pato la mkoa kwa asilimia 75.
“Mkoa wa Ruvuma umeendelea kutekeleza kwa mafanikio Ilani ya uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2015 hadi 2020 kwa kupunguza tatizo la ajira kwa vijana,kuendeleza mapambano dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali za umma na kudumisha amani,ulinzi na usalama wa maisha ya raia na mali zao’’,anasisitiza Mndeme.
Kulingana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012,Mkoa wa Ruvuma ulikuwa na watu 1,376,176 kati yao wanawake 708,207 na wanaume 668.684.Mkoa wa Ruvuma una tarafa 24,kata 173,vijiji 552 na mitaa 95.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini toka Manispaa ya Songea
Septemba 11,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa