KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma (SACP)Gemini Mushy amewaongoza Askari polisi mkoani Ruvuma katika maadhimisho ya miaka 46 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume ambaye aliuawa Aprili 7,1972 ,kwa kutembelea Makumbusho ya Taifa ya Majimaji ya songea ambako kuna makaburi ya mashujaa wa vita ya Majimaji .
Wakiwa katika makumbusho hayo wamefanya usafi wa Mazingira na kupata historia ya mashujaa hao kutoka kwa Mhifadhi Kiongozi wa Makumbusho hayo Balthazar Nyamusya ambaye alieleza mashujaa 66 walinyongwa na kuzikwa katika kaburi la pamoja mwaka 1906 na kaburi moja ni la Nduna Songea Mbano ambaye amezikwa kiwiliwili na kichwa chake kilikatwa na kuchukuliwa na wajerumani ambapo fuvu lake lipo nchini Ujerumani.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa