JESHI la Polisi mkoani Ruvuma limeendelea kufanya misako mbalimbali na kupata mafanikio ikiwemo silaha tano aina ya gobore na mtutu mmoja zilizokuwa zinatumika kinyume cha sheria.Kamanda wa Polisi mkoani ACP Simon Maigwa amesema silaha hizo zilisalimishwa katika ofoso za vijiji mbalimbali kuhofia kukamatwa na polisi na kwamba katika msako huo Polisi walifanikiwa kukamata televisheni nne ambazo ni homebase inchi 32,boss inchi 32 na mr UK nchi 24 pamoja na aborder inchi 24 zote ziliibiwa katika maeneo mbalimbali.
"Natoa wito kwa wananchi kufika kwenye vituo vyetu vya polisi kutambua mali hizo kwa wale waliobiwa,Jeshi la polisi pia tumefanikiwa kukamata jumla ya lita 60 za pombe ya moshi yaani gongo na watuhumiwa wamefikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria'',alisema Kamanda Maigwa.
Kamanda huyo wa Polisi mkoani Ruvuma anatoa rai kwa wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma kujiepusha na vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria za nchi kwa kuwa Jeshi la Polisi litaendelea kufanya msako endelevu kuhakikisha kuwa wanakamatwa wote wanaovunja sheria za nchi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Hata hivyo Kamanda Maigwa amewashauri wananchi kutojichukulia sheria mkononi endepo kunakuwepo na migogoro yoyote ndani ya jamii ni vema kutafuta njia sahihi ya kutatua migogoro hiyo na kwamba amewashukuru wananchi wote ambao ni raia wema kwa jitihada zao za kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kuhusu uharifu na waharifu kwa sababu jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi.
Imeandikwa na Albano Midelo
Afisa Habari Serikalini
Mei 29,2019
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa