Katika kipindi cha mwaka 2022/2023 Serikali ilitenga bajeti ya shilingi Mil. 50 kwa ajili ya kuboresha huduma za utoaji wa mafuta kinga kwa watu wenye ualbino nchini.
Utekelezaji wa huduma mbalimbali nchini umezingatia Sera, Mikataba ya kikanda, na kimataifa na Mipango mbalimbali ya nchi ikiwemo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Sera ya Taifa ya huduma na maendeleo kwa watu wenye ulemavu, sheria ya watu wenye ulemavu namba 9 ya mwaka 2010, na Mkataba wa Kimataifa wa watu wenye ulemavu 2006.
Aidha, Serikali inaendelea kuhimiza Halmashauri zote nchini kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa kinga pamoja na kuongeza wataalamu kwa lengo la kudhibiti saratani ya ngozi kwa watu wenye Ualbino.
Hayo yamejili katika kuadhimisha kilele cha Siku ya Kimataifa ya uelewa kuhusu Albino iliyofanyika kuanzia tarehe 11 juni hadi 13 juni 2023 Mkoani Ruvuma katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa pamoja na wadau mbalimbali kwa lengo la kutoa uelewa kuhusu Albino.
Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Prof Joyce Ndalichako (MB) ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanal. Laban Thomas.
Akizungumza Mkuu wa Wilaya ya Songea Wilman Kapenjama Ndile kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma “ Amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kuhakikisha wanapata takwimu sahihi kwenye maeneo yao za watu wenye Ualbino kwa ajili ya kutoa huduma muhimu.”
Ndile aliongeza kuwa, katika kuimarisha juhudi mbalimbali za ustawi wa jamii kwa watu wenye ulemavu Serikali imechukua hatua za kuwawezesha walemavu kiuchumi pia kwa kutambua juhudi za Serikali katika kushughulikia masuala ya watu wenye ulemavu. “Alibainisha”
“ Serikali inachukua hatua mbalimbali katika kutekeleza matakwa ya kisheria ya watu wenye ulemavu kwa kupitia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025.”
Amewataka kutoa ushirikiano, kujenga upendo na kufanya kazi kwa pamoja ili kuepuka migogoro inayoweza kuleta chuki au kusambaratisha umoja na kuendelea kuchangamkia fursa adhimu ili kujikwamua kiuchumi kwa kufanya marejesho ya mikopo ili kutoa fursa kwa wengine waweze kunufaika.
Alibainisha kuwa Ajira kwa watu wenye ulemavu imesimamia Takwa la 3% kuajiri watu wasiopungua 20 ambapo katika kipindi cha mwaka 2023 Serikali imeajiri watumishi 812 na Intenalship 178.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Vyama vya Walemavu Tanzania ( SHIVYAWATA) Ernest Simaya alisema “ Maadhimisho hayo yalianza mwaka 2006 na hatimaye kuungwa mkono na Mataifa mbalimbali.
Simaya alisema mambo ya msingi ambayo huyashughulikia ni pamoja na suala la ajira kwa walemavu ambapo kwa mwaka 2021/2022 Serikali imeajiri watumishi walimu ( walemavu) 245. “Alibainisha.”
Imeandaliwa na;
Amina Pilly;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa