RAIS wa Tanzania Dk.John Magufuli ametoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya milioni 18 kwa ajili ya zahanati za Halmashauri ya Manispaa ya Songea lengo likiwa ni kuboresha huduma ya afya kwa wananchi.
Vifaa vilivyotolewa ni vitanda 20 vyenye thamani ya shilingi 7,920,000,mashuka 50 yenye thamani ya shilingi 510,000,vitanda vya kujifungulia vyenye thamani ya 6,108,800 na magodoro 20 yenye thamani ya shilingi 3,670,000.
Mbunge wa Songea mjini Dk.Damas Ndumbaro ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Rais kwa uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea katika hafla fupi iliyofanyika katika Kituo cha Afya Mjimwema.
Mbunge wa Songea Mjini Dk.Ndumbaro amesema kukabidhiwa kwa vifaa tiba hivyo ni moja ya ahadi ambazo aliahidi Rais wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Songea Dk.Mameritha Basike amesema vifaa hivyo vitagawiwa katika baadhi ya zahanati zilizopo katika Manispaa hiyo ambazo zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vifaa hivyo.
Imetolewa na Albano Midelo
Afisa Habari Manispaa ya Songea
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa