KATIBU Tawala mkoa wa Ruvuma Prof.Riziki Shemdoe amewataka watumishi wa Umma Mkoa wa Ruvuma kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuharakisha maendeleo na kutoa Huduma bora kwa Wananchi.
Ameyasema hayo katika ukumbi wa kassim Majaliwa uliopo katika shule ya Sekondari Mbamba-bay wakati akiongea na Watumishi wa Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma wakati akiwa katika Ziara ya Siku moja ya kikazi Wilayani hapa.
Shemdoe alifafanua kuwa anawataka watumishi wa mkoa huu wafanye kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa wananchi ili Ruvuma iwe mfano wa kuigwa na isiwe mwishoni inapotajwa kitaifa lengo iwe katika kumi bora na wakuifanya iweze kuvuma kitaifa, ni watumishi wote wa mkoa huu wa Ruvuma kwa kila mtu kuwajibika kwa nafasi yake.
“Niwashukie watumishi wenzangu wa mkoa huu wa Ruvuma na Nyasa kwa ujumla kuwa lengo la Serikali ya awmu ya Tano ni kutoa huduma bora kwa wananchi .Hivyo sisi ni watumishi ambao tumepewa jukumu la kuhakikisha huduma hizo zinatolewa kwa kila mtu kuwajibika vizuri katika nafasi yake kwa kutoa huduma bora mahali pa kazi.Ninahitaji tuwe kumi bora katika shughli zote za Serikali”.
Aliongeza kuwa watumishi wanatakiwa kufanya kazi kwa uadilifu huku wakishirikiana kwa upendo ili kuweza kutatua changamoto wanazozipata kwa ushirikiano kati ya wakuu wa idara mkurugenzi na wakuu wa idara kwa kusimamia uadilifa,uwajibikaji na kushirikiana kujibu hoja za Ukaguzi ambazo zipo katika Halmashauri na eneo la kazi.
“Tuwe na moyo wa upendo kwa kupendana katika kutekeleza majukumu yetu mahali pa kazi kwa ngazi zote kanzia juu mpaka chini ili tuweze kuendelea”
PRO.Shemdoe alibainisha kuwa pamoja na shughuli zingine tunatakiwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kikamilifu ili iweze kuwanufaisha wananchi wote kwa ujumla na kupiga vita Rushwa katika maeneo ya kazi.
Aidha aliwaagiza wakururugenzi kushirikiana na wakuu wa idara na watumishi wa ngazi zote ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kufikia malengo waliyojiwekea katika kutekeleza majukumu yao.
IMEANDALIWA NA
NETHO C.SICHALI
AFISA HABARI
NYASA DC
0783662558
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa