Na;
AMINA PILLY,
AFISA HABARI MANISPAA.
21 DISEMBA 2021.
Mkoa wa Ruvuma wajipanga kukabiliana na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara wa sekta binafsi na umma kwa ujumla.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Generali Brigedia Balozi Wilbert Ibuge katika baraza la wafanyabiashara Mkoani Ruvuma, lilifonyanyika leo tarehe 21 Desemba 2021 katika ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na wafanyabiashara.
Ibuge alisema kuwa baraza la wafanyabiashara la Mkoa wa Ruvuma limefanyika kwa mujibu wa sheria kupitia waraka namba 1 wa mwaka 2001 uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao unaelekeza kufanyika kwa mabaraza kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa lengo la kujadiliana changamoto zinazowakabili wafanyabiashara pamoja na utatuzi.
Ameongeza kuwa baraza hilo linatoa fursa kwa sekta binafsi na umma kujadili kwa pamoja changamoto zinazowakabili na kuzitatua kwa lengo la kukuza uchumi kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Ametoa wito kwa Taasisi binafsi kutumia fursa za kibiashara zilizopo ndani ya Mkoa wa Ruvuma katika uwekezaji, ambapo miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na uchakataji wa asali, utalii, uvuvi, mifugo na kilimo.
Amezitaka Taasisi za Serikali kutoa huduma kwa wafanyabiashara ikiwemo na utoaji wa leseni na vitambulisho, kuboresha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara ikiwemo na miundombinu ya barabara pamoja na kuandaa maeneo stahiki ya kufanyia biashara kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ili kuleta uchumi jumuishi kwa manufaa ya wananchi wote kwa ujumla.
Naye Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Biashara (TMBC) Dr. Godwill Wange amesema kuwa miongoni mwa maazimio yaliyowekwa katika baraza hilo ni pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya msingi ili kufanikisha mazingira stahiki ya biashara hasa kwa wajasiriamalli (machinga), pamoja na Taasisi za uthibiti wa mazingira na OSHA kuhakikisha wana wawakilishi katika kila Wilaya Mkoani Ruvuma kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa wafanyabiashara.
Amesema kuwa wawekezaji wote wanatakiwa kushirikiana kwa pamoja na kuzitumia fursa za kibiashara ambazo bado hazijafunguka ili kujenga viwanda ambavyo vitatumika kutengeneza bidhaa zinazotokana na rasimali zilizopo katika Mkoa wa Ruvuma.
Wange amewataka viongozi wa baraza la Wilaya kuhakikisha wanatatua changamoto za wafanyabiashara kabla ya kuzipeleka ngazi ya Mkoa kwa lengo la kurahisisha utatuaji wa changamoto hizo kwa wakati.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Wakuu wa Wilaya 5, Wakurugenzi wa Halmashauri 8 pamoja na viongozi mbalimbali kwa kuweza kusimamia vizuri utekelezaji wa miradi ya mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO 19 kabla ya wakati uliopangwa na Serikali.
Oddo amewataka viongozi kuhamasisha wananchi kujitokeza kuhesabiwa katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022 nchi nzima kwa lengo la kupata Takwimu sahihi ya idadi ya watu itakayowezesha Serikali kupanga mikakati thabiti kwa maendeleo ya Taifa.’Alisisitiza’
Mwisho.
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa