MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amewashauri wananchi mkoani Ruvuma kujiunga na mfuko wa Bima ya afya ya Jamii CHF ili kuwa na uhakika wa kupata matibabu wanapougua.
Mndeme ametoa ushauri huo wakati anatoa Taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015 kipindi cha Julai, 2017 hadi June ,2018 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho,Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Profesa Riziki Shemdoe,Wakuu wa Wilaya zote tano za Mkoa wa Ruvuma,watalaam ngazi ya Mkoa,viongozi na wajumbe mbalimbali wa CCM Mkoa wa Ruvuma
Mndeme ameagiza watendaji wa Halmashauri zote nane mkoani Ruvuma kuendelea na zoezi la uhamasishaji ili wananchi wajiunge na waendelee kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya.
“kiasi cha fedha zinazochangiwa kwa kila familia au Kaya ni shilingi elfu kumi kwa Halmashauri zote, isipokuwa Halmashauri ya Wilaya Mbinga ambayo kwa mgonjwa wa kulazwa anachangia Shilingi elfu ishirini na shilingi elfu kumi kwa wagonjwa wa nje” amesisitiza Mndeme.
Sekta ya Afya mkoani Ruvuma bado inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kiwango cha maambukizi ya virusi vya UKIMWI cha asilimia 5.5 wakati kiwango cha Taifa cha asilimia 4.7 na pia kutokuwepo kwa vituo vya kutosha vya huduma za afya.
Imetolewa na Viktoria Dejembi
Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Manispaa ya Songea
Septemba 5,2018
SONGEA MUNICIPAL COUNCIL
Anuani ya Posta: P O BOX 14, SONGEA
Simu ya Mezani: 025 2602970
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: info@songeamc.go.tz
Hakimiliki ©2017 Halmashauri ya Manispaa ya Songea. Haki zote zimehifadhiwa